0

                                   
Mwaandishi wetu Kilwa
Jitihada za serikali za kutaka kila shule ya sekondari nchini iwe na maabara kwa masomo ya sayansi zimeendelea kuungwa mkono kwa vitendo.Baada ya shirika la maendeleo ya petroli(TPDC) kutoa msaada wa shilingi milioni 18,kwa halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi,zitakazotumika kwa ununuzi wa vifaa vya ujenzi.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya fedha hizo,yaliyofanyika jana Kilwa Masoko.Afisa uhusiano wa TPDC,Fransis Lupokela,alisema nijambo lisilowezekana kutarajia mafanikio  yanayotokana na matumizi mazuri ya raslimali zilizopo iwapo jamii husika haina elimu.Alisema maendeleo ya kasi na ya haraka yanategemea  kiwango cha elimu ambacho jamii husika inacho,kwani itaweza kuzitambua na kuzitumia fursa zilizopo katika maeneo inamoishi.

Lupokela alisema shirika hilo kama sehemu ya jamii limekuwa linashirikiana kwa ukaribu na wawekezaji ili kuhakikisha jamii inanufaika na raslimali zilizo ikiwamo gesi na mafuta.
Alisema ushirikiano uliooneshwa na wananchi na serikali wilayani Kilwa kwa shirika hilo na wawekezaji katika sekta ya gesi,TPDC linakila sababu ya kubadilisha maendeleo ya wilaya hiyo kwani ni wajibu wake kushiriki kwenye mipango ya maendeleo." baada ya kuona shuguli za shirika zinazidi kupanuka tumeona kuna kila sababu yakuwa na wataalam wanaotoa miongozo na ushauri kuhusu masuala ya jamii, shirika linatarajia kufanya mengi" na kusaidia jamii siyo fedha tu bali kuipa jamii elimu ili iweze kuwa na ujuzi na maarifa ni msaada mkubwa," alisema Lupokela.

Akipokea msaada huo kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilwa,Fransis Kabunda,alisema fedha hizo ambazo zitatumika kununua vifaa vya ujenzi wa vyumba vya maabara za shule za sekondari za Songosongo na Mpunyule.Zimetolewa katika wakati muhafaka kwani utaharakisha ujenzi vyumba hivyo na kutekeleza agizo la serika la kutaka wanafunzi wasome.

.Naye katibu tawala wa wilaya hiyo,Simeon Manjulungu alisema uwekezaji unachochea na kusukuma kwa kasi maendeleo, hivyo wananchi licha kuwa na umuhimu kusimamia rasilimali ili waweze kunafaika,lakini pia wanajiwajibu kutoa ushirikiano kwa wawekezali na kuthamini jitihada zao.
.

Post a Comment

 
Top