0

MBUNGE JOHN KOMBA AFARIKI DUNIA Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ Mikocheni.
Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es salaam.

Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado haijafahamika.
Furahia Maisha Blog imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge ndugu Owen Mwandumbya, Mkurugenzi wa Mambo ya nje na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa hawakupokea simu
 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjpwRcSLaMtgRf7onL1kAPu-UXUVUeAyg2v11W2plMpQi_gcfZgDXZY5MBqWHgx4uuEZ9XjS_C2ps43dSU3eUyA-PlOtBm06QGJaMKeJDd7W4v2Rd6Zwyvt1tabfWJl7wihzrBJfMom4nA/s1600/unnamed+(27).jpg

Post a Comment

 
Top