Wanafunzi ni miongoni mwa wanaoathiriwa kwa kiasi kikubwa na mashambulizi ya Taliban
Wanajifunza namna ya kuweka risasi, kulenga na kufyatua.Silaha wanazotumia ni pamoja na Bastola na Bunduki, pia wanajadili kuhusu mbinu za kujilinda na namna ya kuwalinda Wanafunzi ikiwa Wanamgambo wa Taliban watavamia wakati ambapo watakuwa darasani wakisoma.
Jitihada hizi za mafunzo ya matumizi ya silaha zinatoka katika Serikali ya Jimbo la Khyber-Pakhtunkhwa na Mamlaka ya Polisi, zikiwa ni jitihada za kuimarisha usalama kwenye Shule.
Waziri wa Elimu na Mawasiliano wa Jimbo, Mustaq Ghani amesema Jimbo lina Askari 65,000 lakini hawatoshi kulinda Shule 45,000, taasisi za mafunzo na Vyuo vikuu.
Hatari
ya mashambulizi ya mara kwa mara nchini Pakistani imefanya jamii ya
nchini humo kuchukua hatua ambazo zimeonekana si za kawaida.
Kaskazini
magharibi mwa Pakistani, Polisi wanatoa mafunzo ya namna ya kutumia
silaha kwa Walimu wa shule na Chuo kikuu hatua iliyokuja baada ya
Wanamgambo wa Taliban kuwaua Watu 150 katika Jimbo la Peshawar mwezi
Disemba.Wanajifunza namna ya kuweka risasi, kulenga na kufyatua.Silaha wanazotumia ni pamoja na Bastola na Bunduki, pia wanajadili kuhusu mbinu za kujilinda na namna ya kuwalinda Wanafunzi ikiwa Wanamgambo wa Taliban watavamia wakati ambapo watakuwa darasani wakisoma.

Post a Comment