0
                Mji wa Baga ulioshambuliwa na Boko Haram
Leo ni mwezi mmoja tangu wapiganaji wa Boko Haram waliposhambulia miji ya Baga na Doron Baga kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Idadi kamili ya watu waliokufa haijulikani lakini inadaiwa kuwa ni kati ya watu mia moja na hamsini hadi elfu mbili.
Wakati wapiganaji wa Boko Haram wakivamia kutoka upande wa magharibi wa Baga, kundi la vijana waliodhamiria kupambana na kundi hili walijaribu kuulinda mji wao.
Yalikuwa mafanikio ya nadra kutokea dhidi ya Boko Haram. Kulikuwa na ahueni lakini haikudumu muda mrefu.
Ilikuwa taharuki. Wanawake na watoto, vijana na wazee walizikimbia nyumba zao na biashara, wengi wakikimbilia mji jirani wa uvuvi wa Doron Baga ulio ufukweni mwa Ziwa Chad.Boko Haram waliwafuata Doron.
Iwapo bunduki haikukudhuru, walianza kuua watu kwa kuwagonga na magari yao. Ufyatuaji wa risasi haukuchagua pa kulenga
Mauaji ya Baga na Doron Baga yalitokea mwezi mmoja uliopita…Boko Haram hawakusambaratishwa. Tangu wakati huo, waasi hao wameishambulia miji mingi zaidi kaskazini mashariki mwa Nigeria; watu wengi wamekufa na wengi zaidi wamelazimika kuyakimbia makazi yao.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli amewahakikishia wakazi wa mji wa Tunduma mkoani Mbeya kuwa Serikali itajenga barabara ya njia nne katika mji huo ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji huo kuwa wa kisasa na kibiashara. Amesema hayo katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya barabara inayoendelea katika mikoa ya Mbeya na Rukwa ambapo akiwa mjini Tunduma amekutana na wananchi wanaofanyabiashara katika mji huo. “Dumisheni umoja,amani na mshikamano ili mfanye biashara zenu na kukuza uchumi nasi tutahakikisha tunajenga barabara ya njia nne ili kupunguza msongamano wa magari na kuuwezesha mji wa Tunduma kuwa wa kisasa na kibiashara na hivyo kuwa mahali pazuri pa watu kuishi”,amefafanua waziri Magufuli. Katika ziara hiyo waziri Magufuli amekagua mizani ya Nkangamo na barabara ya Tunduma –Sumbawanga KM 225, iliyojengwa kwa kiwango cha lami na kuwataka wananchi wa mkoa wa Rukwa kutumia barabara hiyo kukuza uchumi wao na wa mkoa wao kwa kufanyakazi kwa bidii. Akihutunbia wananchi wa Sumbawanga Waziri Dkt. Magufuli amewataka wananchi kutambua kuwa barabara za lami zinajengwa kwa gharama kubwa hivyo wazitumie kwa manufaa na wale walioko kwenye hifadhi ya barabara wabomoe nyumba zao mapema ili kuwezesha ujenzi kufanyika kwa wakati. Waziri Magufuli amesema Serikali iko katika hatua za awali kujenga barabara ya Matai-Kasesha KM 50 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha mkoa wa Rukwa nan chi ya Zambia na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza mjini Sumbawanga na hivyo kutoa fursa za ajira na uchumi kwa wananchi. Waziri Magufuli yuko katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya barabara katika mikoa ya Mbeya,Rukwa,Katavi na Tabora ambako kuna miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za lami inayoendelea. Imetayarishwa na kitSengo cha habari na mawasiliano serikalini wizara ya ujenzi.

Copy and WIN : http://bit.ly/copynwin

Post a Comment

 
Top