Wabunge wa bunge la Uingereza wameunga
mkono sheria inayoruhusu uzaaji wa wa watoto wenye vinasaba, DNA kutoka
kwa wanawake wawili na mwaume mmoja, katika tukio la kihistoria.
Uingereza kwa sasa itakuwa nchi ya kwanza kuweka sheria zinazoruhusu watoto wenye vinasaba vya watu watatu tofauti.
Katika kura iliyopigwa katika bunge la
Commons, wabunge 382 waliunga mkono muswada huo wa sheria na wabunge 128
walipinga mbinu inayozuia magonjwa ya kijenetiki kutoka kwa mama kwenda
kwa mtoto.
Wakati wa mjadala huo, mawaziri wamesema mbinu hii ni "mwanga kwa safari ndefu ya giza" kwa familia kupata watoto.
Upigaji kura zaidi unahitajika katika
baraza la bunge la juu, maarufu kama House of Lords. Iwapo kila kitu
kitakwenda sawa, basi mtoto wa kwanza wa teknolojia hii atazaliwa mwaka
ujao.
Watetezi wa mpango huu wanasema uungwaji
mkono wa sheria hii "ni habari njema kwa maendeleo ya tiba" lakini
wakosoaji wanasema wataendelea kupinga mpango huu ambao una mashaka
mengi kuhusu maadili na usalama katika uzazi huu.
Makisio yanasema watoto 150 wanaopatikana kutokana na vinasaba vya watu watatu watazaliwa kila mwaka.
Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron
anasema: "Hatuzungumzii Mungu hapa, tunahakikika kuwa wazazi wawili
ambao wanataka mtoto mwenye afya wanaweza kumpata."
Mpango huu ambao umebuniwa Newcastle,
utasaidia wanawake kama Sharon Bernardi, kutoka Sunderland, ambaye
alipoteza watoto wote saba kutokana na ugonjwa wa mitochondrial.CHANZO:BBC

Post a Comment