0
                          
 Misri imemfungua na kumsafirisha mwandishi wa habari wa Al Jazeera, Peter Greste, ambaye alifungwa kwa kushirikiana na kundi lilopigwa marufuku.Ameondoka Misri kwenye ndege iliyokuwa inaelekea Cyprus.
Inafikiriwa atakwenda kwao Australia.
Al Jazeera imekaribisha kufunguliwa kwa Bwana Greste baada ya kifungo cha siku 400, lakini imeomba kuwa wenzake wawili, Mohamed Fahmy na Baher Mohamed, piya wasamehewe.
Duru katika ikulu ya Misri zinasema kuwa Mohamed Fahmy -- mwenye uraia wa nchi mbili, ataondoshwa ili kupelekwa Canada pale uraia wake wa Misri utapofutwa.
Waandishi hao wa habari watatu walihukumiwa kifungo baada ya kesi ambayo watu wengi wamelalamika kwamba haikuwa sawa.
Kulikuwa na kampeni ya kimataifa kujaribu kufanya wanaume hao wafunguliwe.

Post a Comment

 
Top