wajumbe wa baraza la madiwani halmashauri ya wilaya kilwa mkoani Lindi wakiwa kikaoni cha bajeti
mwanasheria wa halmshauri ya wilaya kilwa na afisa utumishi wakiwa kwenye kikao cha baraza la madiwani wakifuatilia kikao hicho kwa umakini
Mwaandishi wetu Kilwa
Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoa wa Lindi, lilipitisha mpango wa makisio ya bajeti mwenye jumla ya shilingi bilioni 27.4 kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016.
Akisoma bajeti hiyo Mkurugenzimtendaji wa
halmashauri hiyo,Maimuna Mtanda alisema katika kipindi hicho halmashauri hiyo
itahitaji kuwa na jumla ya shilingi 27,419,533,212.00 ambazo zitatumika katika
kutekeleza miradi ya maendeleo na matumizi ya kawaida(mengineyo) na mishahara
ya watumishi.
Mtanda alisema bajeti hiyo ina ongezeko
la shilingi 6,420,907,082.00 sawa na asilimia 30.6 ya bajeti ya
mwaka 2014/2015 kutokana na ongezeko la mishahara yenye jumla ya shilingi
6403484812.00,sawa na asilimia 58.8 ya mishahara ya bajeti iliyopita,na
ongezeko la mapato ya ndani lenye jumla ya shilingi 17,422,270.00.
Alisema kuwa fedha hizo zitatokana na makusanyo
kwenye vyanzo mbalimba ikiwa ni pamoja na ruzuku ya mishahara shilingi
18,300,146,812.00,ruzuku ya matumizi mengineyo shilingi 1,617,843,000.00,ruzuku
ya miradi ya maendeleo shilingi 3,161,080,000.00,mapato ya ndani shilingi
2,823,047,400.00 na misaada kutoka kwa wahisani na marafiki wa maendeleo
shilingi 1,472,416,000.00
Mtanda alisema ili kuongeza kiwango cha
mapato ya ndani Halmashauri hiyo imeandaa mikakati ya ukusanyaji mapato,ikiwamo
kuanzisha kikosi kazi cha ukusanyaji mapato,kuongeza wigo wa kubuni vyanzo
vipya vya mapato,kuongeza viwango vya kodi katika baadhi ya vyanzo vya mapato
na kuimarisha rejesta za vyanzo mbalimbali vya mapato.
Mkurugenzi hiyo alisema katika matumizi ya shughuli
za maendeleo kipaumbele kitakuwa kutekeleza miradi ya maji, kwani katika wilaya
ya hiyo ni asilimia 47 ya wananchi wanaopata na kutumia maji safi na
salama
Kwa upande wake katibu tawala msaidizi wa
mkoa Lindi,Abdallah Dachi aliitaka halmashauri hiyo kuwa na udhibiti na
ukusanyaji wa mapato,ambapo pia aliitaka kuipa vipaumbele miradi ambayo
haijakamilika(viporo)
Post a Comment