0
         Madiwani Nachingwea mkoani Lindi wakiwa kwenye kikao za bajeti

 Tuwahurumie viongozi wa vitongoji na na vijiji , maneno ya Diwani wa Mnero mathew
Afisa mipango wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Mnunduma akiwa kwenye kikao cha madiwani cha bajeti 

NACHINGWEA  YAPAA  KUKUSANYA,KUTUMIA BILIONI 31 .7/-MWAKA 2016
 Mwaandishi wetu Nachingwea

WAJUMBE wa baraza la madiwani Halmashauri ya Wilaya  Nachingwea Mkoani Lindi  limepitisha bajeti ya zaidi ya sh bilioni 31.7 zitakazokusanywa na kuelekezwa katika utekelezaji wa miradi  ya maendeleo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2015/2016.
Kati ya kiasi hicho cha fedha,sh bilioni 2.237zinatarajiwa kukusanywa kutoka kwenye vyanzo vyake mbalimbali vya  mapato ya ndani ambapo ruzuku kutoka serikali kuu na misaada kutoka kwa wafadhili ikitarajiwa kuwa ni zaidi ya sh bilioni 9.44
Akisoma taarifa ya mapendekezo ya mpango wa maendeleo na bajeti ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea kwa mwaka wa fedha mwaka 2015/2016 katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo,Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Valery Kwembe  alisema makadilio ya bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 ni sh bilioni 31.762.
Alisema makadilio hayo yamepanda kutoka sh bilioni 22.568 kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015 ingawa hadi kufikia Novemba 2014,Halamashauri hiyo ilifanikiwa kukusanya jumla sh bilioni 9.260 kati ya bilioni 10.080 zilizokusanywa sawa na asilimia 92%ya makadirio.
Kwa mujibu wa Kwembe Halmashauri inatarajia kutumia bilioni 9.443 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kutumia vyanzo mapato kama vile ruzuku kutoka serikali kuu,vyanzo vya ndani pamoja na fedha kutoka kwenye programu za Elimu  Sekondari (SEDP),Maji na Usafi (NWSSP) ruzuru ya maendeleo ya serikali za mitaa(LGCDG) Mpango shirikishi wa misitu(PFM)pamoja na Mfuko wa Barabara.
Kwembe alisema licha ya kupitisha makisio ya bajeti ya mwaka wa fedha wa 2015/2016 Halmashauri hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ambazo huathiri utekelezaji wa malengo wa yanayowekwa kama vile kucheleweshwa kwa fedha za ruzuku kutoka serikali kuu, pamoja kutofikiwa kwa malengo ya ukusanyaji mapato kwenye baadhi ya vyanzo vya Halmashauri.
Kwa upande mwenyekiti wa halmsahauri hiyo Abdala Chikawe aliwataka madiwani kushirikiana na watendaji katika kukusanya mapato  kupitia vyanzo vya ndani vya halmashauri ili kufikia malengo wajiojiwekea.
Chikawe  alisema kama madiwani na watendaji wa vijiji, na kata watashirikiana katika kukusanya  mapato kwa uadilifu  katika maeneo hayo  kutaweza kusaidia kuongezeka kwa mapato ya halmsahuri  hiyo.

Post a Comment

 
Top