mwaandishi wetu Liwale……
Wakulima wa wilayani liwale wameiomba serikali kuvitumia vyama vya
ushirika kusambaza pembejeo za ruzuku ili kupunguza urasimu na kuchelewa kuwafikia wakuilma kwa wakati
unaofanya na mawakala wanao sambaza kwa
wakulima.
Ombi hilo metolewa
na wakulima wa korosho wa chama cha ushirika Mida kata ya mihumo wilayani Liwale mkoa Lindi
wakati walipokuwa wanazungumza na timu ya waandishi wa habari waliotembelea
chama hicho .
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa bodi ya
ushirika ya chama hicho Rashidi mpuke na
Tabia Mbanila alisema kitendo cha mfuko
wa kuendeleza zao la korosho kusambaza
pembejeo kuwatumia mawakala
kumechangia wakulima kuchelewa
kupata pembejeo hizo na kwa kiasi kidogo
tofauti na mahitaji ya wakulima
Rashidi Mpuke
alisema msimu 2013/14 uzalisha
ulipungua kutokana na kuchelewa kwa
pembejeo hali iliyotokana na wakulima kuutegemea
mfuko wa pembejeo kuwasambazia mpembejeo
hizo kwa wakati.
Tabia mbanila alisema kuwa ukosefu wa elimu juu ya mfumo wa stakabadhi ghalani ni moja ya
chngamoto zinazowakabili wakulima wakorosho
na kusababisha kuilalamikia serikali
kuwa inawatelekeza wakulima hao.
Mbanila alisema kama serikali ingetoa elimu juu ya mfumo matatizo mengine
yangepungua kwani mfumo kwa ujumla ni
mzuri na ni mkombozi kwa wakulima wa mazao ya korosho.
Post a Comment