0

                                   sherehe za ushindi zilikuwa hivi

                                       katibu wa ccm wilaya ya liwale mwanamke aliyekatikati 

mwaandishi wetu liwale
Mbunge wa Liwale mkoani Lindi Faith Mitambo amewashukuru wananchi wa jimbo lake la uchaguzi kwa kukipatia ushindi wa kishindo Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uchagfuzi wa Serikali za Mitaa mwishoni mwa mwaka jana sherehe hizo zilifanyika katika kijiji cha lilombe.
Mitmbo alitoa pongezi hizo jana wakati akizungumza na mdau wetu kuhusu matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika kote nchini Desemba 14,mwaka jana.
Nawashukuru sana wananchi wa jimbo la uchaguzi Liwale kwa ushindi wa kishindo walioupatia chama chetu cha mapinduzi katiaka uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Nina kila sababu ya kuwashukuru kwa sababu wameonesha imani kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM),lakini kubwa ushindi huo ni kutokana na kutekelezwa vyema kwa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 hadi 2015,alisema Mitambo.
Katika uchaguzi huo wa katika jimbo la Uchaguzi la Liwale,CCM ilishinda kwa wastani wa jumla ya asilimia 57,ikiwa na maana imevuka wastani wa wapinzani wake, kama alivyoeleza juzi katibu mkuu wa CCM Abdurahman Kinana akiwa ziarani Tanga.
Katika jimbo la Liwale,ccm imeshinda vijiji 39 na vitongoji 181, na chama cha wananchi (CUF)  vijiji 37 na vitongoji 161, chadema vitongoji 8 NCCR Mageuzi  Kitongoji  kimoja.

 Mitambo ambae ni mwanasiasa mwanamama  ni miongoni mwa wanaCCM  na wabunge wanaotajwa kuwemo katika mbio za kuwania na kutetea viti  vyao  vya Ubunge katika uchaguzi unaotarajiwa  kufanyika baadaye  mwaka huu.

Post a Comment

 
Top