Alliance for Change and Transparency
(ACT-Tanzania)
______________________________ _____
Maazimio ya Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania kufuatia Mkutano wake wa Pili Uliofanyika Jumatatu Tarehe 12 Januari 2015 katika Hoteli ya Kagame, Jijini Dar es Salaam
Halmashauri Kuu ya ACT-Tanzania
ilifanya Mkutano wake wa Pili wa kawaida siku ya Jumatatu tarehe 12
Januari 2015 katika Hoteli ya Kagame Jijini Dar es Salaam. Pamoja na
mambo mengine, Halmashauri Kuu ilipokea na kujadili taarifa mbalimbali
na kutoa maamuzi na maazimio katika mambo mbalimbali kama ifuatavyo:
1. Halmashauri Kuu ilipokea, kujadili na KUPITISHA k Mwongozo na Kanuni
za Uchaguzi ndani ya Chama cha ACT-Tanzania. Halmashauri Kuu imepanga
uchaguzi ndani ya chama ufanyike kuanzia tarehe 17 Januari 2015 katika ngazi ya Shina na kukamilika tarehe 28 Machi 2015 katika ngazi ya Taifa.
2. Halmashauri Kuu ilipokea na kujadili Taarifa ya Kamati Maalumu ya
Nidhamu iliyoundwa na Kamati Kuu kuchunguza masuala ya nidhamu ya
viongozi wa Kitaifa, ambao ni Mwenyekiti wa Muda wa Taifa Ndugu Kadawi
Lucas Limbu na Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold Mahona. Baada ya mjadala
wa kina na kuridhishwa na makosa yaliyotendwa na viongozi hawa,
Halmashauri Kuu imetoa maamuzi yafuatayo:
a. Imemsimamisha Ndugu Kadawi Lucas Limbu katika nafasi yake ya Mwenyekiti wa
Muda wa Taifa baada ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani na wajumbe 57 (87.7%)
kati ya wajumbe 65 waliohudhuriwa.
b. Imemwondoa katika nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu Ndugu Leopold Mahona
baada ya wajumbe 57 (87.7%) kupiga kura za kuunga mkono pendekezo hilo kati ya
wajumbe 65 waliohudhuria.
3. Halmashauri Kuu imeazimia kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu
wa mwaka huu na imeagiza Kamati Kuu kujiandaa na uchaguzi huo katika
ngazi zote.
Pamoja na salamu za uzalendo za ACT-Tanzania
Samson Mwigamba
Katibu Mkuu ACT-Tanzania.
Post a Comment