mwaandishi wetu Liwale.
Chama cha
kuuza na kununua mazao Umoja wilayani Liwale mkoani Lindi kimeanza
kutekeleza mradi wa kugawa mbegu za Alizeti zenye thamani ya shs
milioni 6 kwa wakulima zaidi ya 700 kwa lengo la kuinua
uchumi kwa kulitumia zao hilo kuwa zao mbadala badala ya korosho na ufata
.
Hayo
yamebainishwa na mwenyekiti wa chama hicho Hasani Mpako
wakati wa hafla ya uzinduzi wa mpango huo Uliofanyika
katika ukumbi wa Tengeneza wilayani hapa mwi mwazoni mwa wiki hii.
Mpako
alisema wakati wa utekelezaji wa mradi huo
wakulima watafaidika kutokana na uwezeshwa wa kiteknolojia ili
kuweza kupata mazao mengi sambamba na kupata mashine na
utaalamu wa utayarishaji wa mafuta ya alizeti.
Alisema mradi huo
utatekelezwa kwa hawamu ya kwanza katika kata tatu za majaribio ambazo ni
kata za Nangando, Liwale, na Likongowele ambapo pamoja na mambo mengine
kwa lengo la kubaini na kupunguza vikwazo na changamoto
wanazozipata wakulima wa korosho ili waone namna ya kutumia fursa
hiyo badala ya kuendelea kuilahumu serikali kwa kukosa soko la
zao la korosho ambalo limekuwa zao kuu lakini soko lake halina uhakika wa bei na bei yake ipo chini hivyo haileti tija kwa wakulima ukilinganisha na ghalama za pembejeo.
Post a Comment