Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
Mbunge wa jimbo la Uzini na mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha mapinduzi
Mh. Mohamed Seif Khatib mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Dunga
wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja akiwa katika ziara yake ya kikazi
akikagua na kuhimiza utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama hicho ya
mwaka 2010, Katika mikutano mbalimbali ambayo Kinana amekuwa akihutubia
na kuzungumza na wananchi na wana CCM amekuwa akihimiza viongozi kufuata
maadili ya uongozi jambo ambalo ni muhimu na la lazima katika uongozi
ili kuutumikia umma katika misingi mizuri na yenye tija,Katika
ziara hiyo Kinana amewahimiza Wazanzibari kuipigia kura ya ndiyo Katiba
mpya iliyopendekezwa kwakuwa inatatua kero nyingi za wanzanzibari
katika muungano na kuwafanya wawe na uhuru zaidi , kama vile Rais wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwa makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania iwapo Rais wa Jamhuri atatoka Bara, Zazibar
kujiunga na jumuiya za kimataifa bila kikwazo, kuwa na uhuru wa kukopa
na mambo mengine mengi yaliyomo katika katiba hiyo.(PICHA NA KIKOSIKAZI
CHA FULLSHANGWE-UZINI-ZANZIBAR)
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakati alipowasili katika kijiji cha Dunga jimbo la Uzini mkoa wa Unguja Kusini leo.
Mh.
Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za
vijana wa pili kutoka kushoto akiwa katika mkutano wa ndani pamoja na
wawakilishi wenzake wakati wa mkutano wa ndani uliofanyika kijiji cha
Dunga. Ndugu
Sauda Mpambalyoto Katibu wa CCM wilaya ya Kati mkoa wa Unguja Kusini
akisoma taarifa ya utekelezaji ya chama cha mapinduzi mbele ya Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana wakati wa mkutano wa ndani
uliofanyika kijiji cha Dunga leo.Kutoka kulia ni Balozi Ali Karume na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Dkt. Mahadhi Juma Maalim wakiwa katika mkutano huo.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Unguja kusini.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na
Naibu Katibu Mkuu Bara Ndugu Vuai Ali Vuai kumwaga zenge la linta kwenye
jengo la CCM Dunga.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa soko la samaki huko Unguja Ukuu jimbo la Koani.Baadhi
ya wana CCM wakifurahia wakati wa mapokezi ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana wakati alipowasili katika soko la Unguja Ukuuu jimbo
la Koani.Mwakilishi wa jimbo la Chwaka Mh. Issa Haji Gavu akizunguza wakati alipokabidhi misaada mbalimbali katika jimbo lake la Chwaka.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi jenzi kwa vijana wa jimbo la Chwaka.Injinia
Heri Tumaini Mkurugenzi wa kampuni ya CHECOTEC (T) LTD inayojenga
barabara katika jimbo la Chwaka akishukuru na kuzungumza maneno yenye
hisia ya furaha yake kwa kukutana na katibu Mkuu wa CCM Ndugu
Abdulrahman Kinana.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kazi ya
kupanda miti katika shamba la viungo la Alis Spices &Fruits Farm
wakati alipokagua shughuli zinazofanywa katika shamba hilo lililopo
Kwabani jimbo la Koani Zanzibar.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia miche ya mikarafuu.Mmiliki wa shamba hilo Bw. Ali akizingumza na kumshukuru katibu mkuu wa CC kwa kutembelea shamba hilo.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga picha ya
pamoja na mmiliki wa shamba hili pamoja na wafanyakazi.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akipanda kwenye
tanki la maji wakati alipotembelea na kukagua mradi huo uliopo kijiji
cha Michui jimbo la Koani Zanzibar.Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi
katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni jimbo la
Uzini.Baadhi ya wananchi wakinyoosha mikono yao kuashiria kuiunga mkono na kuipitisha Katiba mpya iliyopendekezwa.Mbunge
wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib akiwahutubia wananchi wa
jimbo la Uzini katika mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Tunduni.Baadhi
ya wawakilishi wa timu mbalimbali wakiwa na jenzi zao zilizokabidhiwa
na mbunge wa jimbo la Uzini Mh. Mohamed Seif Khatib.Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na
wananchi katika kijiji cha Tunduni wakati wa mkutano wa hadhara,Mh.
Wanu Hafidh Ameir Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Mwakilishi nafasi za
vijana wa kwanza kutoka kushoto akiwa na wawakilishi wenzake
wakifuatilia mkutano huo uliofanyika kijiji cha Tunduni.Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya waliojiunga na chama hicho.
Post a Comment