0

Kesi ya Feisal Mohammed anayeshukiwa kuwa mlanguzi mkubwa wa Pembe za ndovu Afrika Mashariki inatarajiwa kuendelea hii leo jijini Mombasa. Feisal amekuwa rumande kwa majuma mawili sasa baada ya kunyimwa nafasi ya kuachiliwa kwa dhamana.
Feisal Mohammed anatarajiwa kuanza kujitetea mbele ya Mahakama ya Mombasa , dhidi ya mashtaka ya kumiliki na kulangua kilo 314 ya pembe za ndovu zilizopatikana bandarini Kenya. Ameshinda akila maharagwe tangu Desemba baada ya mahakama kukataa kumwachilia kwa dhamana wiki mbili zilizopita, ikisema kuna uwezo atahepa nchii hii Kesi yake ikiendelea. Mshukiwa alikamatwa nchini Tanzania Desemba mwaka jana, miezi sita baada ya kesi yake kuanza, huku upande wa mashtaka ukisema alitorokea huko baada ya kuarifiwa kuwa anatafutwa na Polisi. Feisal Mohammed ametajwa na Polisi wa Kimataifa Interpol kama mkuu wa kikundi sugu kinacholangua pembe za ndovu.KWA HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

Post a Comment

 
Top