Mateka wakiwa wamepigishwa magoti tayari kwa
kuuawa.
Mateka wakipelekwa sehemu ya kuadhibiwa kwa ujasusi
dhidi ya ISIS.
Baadhi ya wanajeshi wa usalama wa ISIS wakionyesha
bastola zao.
Namna ambayo wapiganaji wa ISIS huvaa nguo zao.
WAPIGANAJI wa Taifa la
Kiislam (ISIS) lililoanzishwa katika maeneo ya Syria na Iraq, wametoa picha za
maofisa wanane wa polisi wa Iraq waliokamatwa na kuuawa kwa kufanya ujasusi
dhidi ya ISIS kwa ajili ya serikali ya Iraq.
Kwa mujibu wa habari kutoka Taifa la Kiislam,
kiongozi wa watu hao alitajwa kama Kepteni Hossam Salah Bnosh ambapo yeye na
wenzake walibadili madhehebu yao na kujiunga na madhehebu ya Kiislam ya Sunni,
lakini baadaye wakachukua fursa hiyo kufanya ujasusi dhidi ya ISIS.
Mauaji hayo ambayo yalifanyika mchana, yalikuwa na
lengo la kuwaonyesha walimwengu adhabu hiyo iliyotolewa kwa watu hao ambao
walikuwa wamevishwa ‘magwanda’ ya rangi ya chungwa kama wavaayo wafungwa wa
gereza la Guantano linalomilikiwa na Marekani huko Cuba.




Post a Comment