Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA) imesema mikoa yote ya Tanzania itakuwa imeunganishwa kwenye mfumo
wa dijitali ifikapo Machi mwakani.
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma,
aliyasema hayo jana ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mkutano wa siku
moja kuadhimisha Siku ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) ya
Jumuiya ya Mawasiliano Afrika (ATU).
Alisema mikoa iliyokuwa imesalia ya Ruvuma,
Mtwara, Iringa na Lindi licha ya baadhi ya wananchi wake kupata huduma
za matangazo kupitia visimbuzi mbalimbali lakini bado haijaingizwa rasmi
katika mfumo huo.
Kukamilika kwa huduma hiyo katika mikoa hiyo
kutafanya nchi nzima sasa kupata huduma za kidijitali ambayo inalenga
kuwasaidia wananchi kupata matangazo bora.
Kuhusu mkutano huo unaotarajiwa kufanyika Desemba
4, mwaka huu, Profesa Nkoma alisema, lengo lake ni kuwakutanisha wadau
kutoka ndani na nchi ya nje kubadilishana uzoefu wa namna ya kuboresha
huduma za sekta hiyo.
“Zaidi ya washiriki 200, wanatarjiwa kushiriki
mkutano huo. Mwingine umefanyika jana Desemba 5, mwaka huu uliohusisha
watangazaji wa televisheni.”
Post a Comment