0


Wafanyabishara wawili wa hapa Liwale mjini bwana Mohamedi Khalifa na Mr Lingindo kwa pamoja  wameuunga mkono kwa vitendo kwa kutoa msaada wa mifuko ya saruji 102  katika kuchangia ujenzi wa maabara,kupitia kwa mhamasishaji mkuu wa zoezi hilo ambaye ni mkuu wa wilaya bwana Ephraim Mmbaga amepokea mifuko 70 ya saruji yenye  kutoka kwa bwana Mohamedi Khalifa.Pia amepokea mifuko ingine ya saruji  32  kutoka kwa Mr.Lingindo,Zoezi la kukabidhiwa saruji limefanyika hii leo.

Mkuu wa wilaya amebainisha mgawanyo wa seruji hiyo,Shule zilizonufaika na msaada huu ni shule ya sekondari Mirui,Kiangara,Likongowele,Nangando na mifuko 8 imepata Liwale High school na amewashukuru sana kwa michango yao  waliyotoa pia ametoa wito kwa wengine waige moyo huo wa kizalendo na amewaomba wanaliwale walio nje ya Liwale na watu wenye uwezo  kuchangia zoezi hili kwa faida ya watoto wetu pamoja na jamii nzima.



Post a Comment

 
Top