Usiri katika mikataba ya utafiti na uchimbaji wa gesi umesababisha Jeshi la Polisi kuwatia mbaroni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) (pichani kulia) na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika hilo kwa kukaidi agizo la kuwasilisha mikataba hiyo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC).
Mwenyekiti huyo, Michael Mwanda na Kaimu Mkurugenzi, James Andilile, walitiwa mbaroni jana jijini Dar es Salaam
baada ya Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe, kutoa taarifa polisi baada ya
menejimenti ya TPDC kukaidi agizo la kukabidhi mikataba hiyo kwa PAC.
Kabla ya
kukamatwa, viongozi hao waliingia katika kikao cha PAC na Mwenyekiti wa
kamati hiyo, Zitto na Makamu wake, Deo Filikunjombe, walitaka kujua
sababu zilizowafanya washindwe kuwasilisha mikataba hiyo wakati ni haki
ya kisheria wabunge kuiona na kuikagua kwa niaba ya wananchi.
Katika kikao
hicho Andilile alionekana kuzidiwa maswali aliyokuwa akiulizwa na
wajumbe wa kamati hiyo na kuanza kujibu kana kwamba hana uhakika na
alichokuwa akikijibu.
Baadaye ilifika
zamu ya Mwanda aliyetakiwa kujibu sababu za kutopeleka mikataba hiyo.
Aliitupia mzigo Wizara ya Nishati na Madini pamoja na Mwanasheria Mkuu
wa Serikali kwamba waliandika barua ofisi zote mbili kuomba mwongozo
kuhusu ombi la PAC kutaka kupitia mikataba ya gesi.
Mwenda aliongeza kuwa licha ya jitihada zilizofanywa na TPDC kuomba mwongozo huo kwa wizara hawakujibiwa hadi jana.
Baada ya
mahojiano hayo, Zitto akizungumza na waandishi wa habari alisema TPDC
wameonyesha dharau kwa Bunge kwa kukaidi agizo halali la kamati hiyo la
kutakiwa kupeleka mikataba 26 ya gesi ili kujiridhisha juu ya uhalali
wake pamoja na manufaa yake kwa Watanzania.
Naye
Filikunjombe alisema uongozi wa TPDC umeonyesha dhahiri kuwatetea
wawekezaji badala ya kujali maslahi ya taifa na kwamba kamati hiyo kamwe
haitakubali na wabunge wataendelea kutimiza wajibu wake.
Hata hivyo, dalili za kukamatwa kwa viongozi hao zilionekana mapema asubuhi kutokana na askari kuonekana maeneo ya ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam na kuruhisiwa kuingia katika kikao hicho.
Baada ya
askari kuingia ndani ya kikao, waandishi wa habari walitolewa nje na
baada ya muda mfupi ndipo Mwenyekiti wa Bodi ya TPDC na Kaimu Mkurugenzi
walipowekwa chini ya ulinzi na kuchukuliwa toka katika ofisi za Bunge
kupelekwa kituo cha polisi kati.
WAACHIWA HURU
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
jana jioni alisema Jeshi la Polisi limewaachia huru Mwanda na Andilile
kusubiri ufafanuzi wa Bunge kuhusiana na tuhuma zinazowakabili.
“Tumeona hakuna sababu ya kuendelea kuwashikilia viongozi hao na badala yake wameachiwa huru tukisubiri taratibu na sheria,” alisema.
Alisema
tukio la kukamatwa kwa viongozi hao lilitokea jana saa 5:00 asubuhi
katika ukumbi wa Bunge, jijini Dar es Salaam katika chumba cha mikutano
ambako kulikuwa na kikao cha PAC.
Kamishna Kova alisema katika kikao hicho ajenda ya mkutano ilikuwa ni kuwasilisha mahesabu ya TPDC katika kipindi kinachoishia 30 June,
2013 na baada ya majadiliano ya muda kuhusu hati mbalimbali
zilizotakiwa na PAC hatimaye Zitto alitoa agizo kwa askari waliokuwapo katika eneo hilo wawakamate vigogo wa TPDC.
“Kutokana na
maelezo ya mashahidi waliokuwapo kwenye tukio hilo katika ukumbi wa
Bunge, Mwenyekiti Zitto alisema wapelekwe Polisi waende kusubiri
mwongozo wa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambaye atawasiliana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa maagizo ya
mwisho,” alisema.
Alisema
baada ya agizo la Zitto vigogo hao wa TPDC walikamatwa na kufikishwa
kituo cha Polisi Kati chini ya ulinzi, lakini Jeshi la Polisi Kanda
Maalum ya Dar es Salaam lilishindwa kuchukua hatua kwani shauri hilo
halikuwa na mlalamikaji alikwenda kufungua jalada na kutoa ufafanuzi
kuhusu mashtaka yanayowakabili viongozi hao.
Aidha, maofisa wawili wa sekretarieti ya Bunge waliitwa Polisi kutoa ufafanuzi kuhusu kadhia hiyo wakiwapo
mawakili wa watuhumiwa na hatimaye kilifanyika kikao cha dharura ili kupata ufafanuzi wa kisheria.
pia
Kova alisema
iligundulika kwamba katika Sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge
sura ya 296 Kif 12 (3) kinaonyesha kwamba Mwenyekiti wa PAC alitakiwa
kwanza apendekeze kwa Spika wa Bunge juu ya jambo lolote aliloliona
kama ni kosa.
Alisema kwa
mujibu wa utaratibu, Spika akisharidhika kuhusu tuhuma zozote
zilizoletwa mezani kwake na Mwenyekiti wa PAC, ndipo anamwandikia
Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili suala hilo lipate ufafanuzi wa kisheria
ikiwa ni pamoja na hatua za kisheria zinazostahili kuchukuliwa.
Kova alisema
katika kikao hicho na jopo la wanasheria iligundulika kwamba katika
sheria ya Haki, Kinga na Madaraka ya bunge, agizo la kukamatwa viongozi
wa TPDC lililotolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge lilihitaji
kuzingatiwa kwanza kabla ya utekelezaji wake.
Mwaka jana
PAC ilitoa agizo kwa menejimenti ya TPDC kuwasilisha mikataba ya utafiti
na uchimbaji wa gesi 26 kwa kamati ili ikaguliwe, katika kikao baina
yao mwaka huu.
Hata hivyo,
Oktoba 28, mwaka huu menejimenti ya TPDC ikiongozwa na Mwanda,
ilihudhuria kikao hicho bila ya kuwa na nyaraka hizo muhimu, kinyume cha
maagizo ya kamati hiyo.
Hivyo,
akasema kama PAC wanahitaji nyaraka hizo, basi wanatakiwa wamwandikie
waziri huyo kumuomba awapatie na siyo kuwabana TPDC wafanye hivyo.Waziri
wa Nishati na Madini, alifanya mkutano na wajumbe wa bodi ya TPDC,
Septemba 15 mwaka jana na kuwaagiza kupitia upya mikataba, ambayo
tayari ilishaingiwa na kuwakataza kusaini mikataba mipya hadi
watakapokuwa wametoa ripoti ya mikataba hiyo.
habari naTHOBIAS MWANAKATWE
CHANZO - NIPASHE
Post a Comment