0

Waziri wa Madini na Nishati, Profesa Sospeter Muhongo.
 WABUNGE kwa pamoja wamekubaliana kuondoa maazimio 12 yaliyoletwa bungeni na Kamati ya PAC na kuleta maazimio mapya 8 ambayo yamekubaliwa.
 
Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Jaji Frederick Werema.
 Mojawapo ya maazimio hayo ni Mamlaka ya uteuzi kutakiwa iwawajibishe na kushauriwa kutengua uteuzi wa Waziri wa Nishati na Madini Profesa Muhongo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Prof. Anna Tibaijuka na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi kwa kuhusika katika sakata la akauntii ya Tegeta Escrow. 


Bunge limeanza saa 1 kamili jioni 
Naibu Waziri wa Sheria: Ameomba kuondoa hoja za serikali zilizoletwa bungeni jana ziondolewe. 
Lissu: Anaomba kuondoa hoja alizowasilisha Mnyika: Naye anaomba kuondoa hoja alizowasilisha
Zitto naye ameomba kuondoa maazimio yote 12 yaliyoletwa bungeni na kamati ya PAC jana ili aweze kuleta maazimio mapya 8
 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka.
 Spika anakubaliana na wajumbe na kuliomba bunge kusema kama wanakubaliana nao au la
 Wabunge wanakubaliana na wenzao kuondoa maazimio hayo ya jana.
Zitto anaanza kuwasilisha maazimio mapya 8 ya PAC kuhusu Sakata la Tegeta Escrow.
 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
 MAAZIMIO MAPYA
 -Serikali ipitie upya mikataba ya Umeme na itoe taarifa kabla ya kumalizika kwa mkutano ujao wa bunge la Bajeti
-Kwa kuwa majaji walihusika, Rais aunde Tume ya kijaji ya uchunguzi na kuwasimamisha jaji Mujulusi na Prof Luhangisa 
-Mamlaka husika ziitangaze Benki ya Stanbic na benki yoyote nyingine itakayogundulika kuwa zinahusika na utakatishaji 
-Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge 
-Bunge liwawajibishe wabunge ambao ni sehemu ya bodi ya TANESCO na viongozi wa Kamati za Bunge 
-Mamlaka ya uteuzi iwawajibishe na inashauriwa kutengua uteuzi wa Prof Tibaijuka, Prof Muhongo, Jaji Werema, Maswi

Mbowe: Naunga mkono Azimio hili, na ninamuomba Waziri Mkuu awe makini katika kutimiza majukumu yake na kusimamia mambo yaliyo chini yake
Filikunjombe: Nawashukuru wabunge wenzangu kwa ushirikiano, nafurahi kuona hatua zimechukuliwa kwa kuwa makosa yamefanyika  
Waziri Mkuu: Amekubali kuwa maazimio yote 8 yatafanyiwa kazi ipasavyo na kulifunga bunge rasmi mpaka Januari 27, 2015.
 Spika Makinda: Wakati wa kuhitimisha shughuli za bunge amewataka wajumbe kuwa makini na watu wanaowatafuta na kuwalaghai na fedha zao!

Post a Comment

 
Top