0

Kumetokea shambulizi katika shule moja ya upili wakati watoto wakiwa wamekusanyika shuleni humo mjini Potiskum Kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Hata hivyo hakuna taarifa kamili kuhusu idadi ya majeruhi kufikia sasa.
Mlipuko huo ulitokea katika shule ya mafunzo ya sayansi ya vijana mjini humo.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu Boko Haram huenda ndilo limefanya shambulizi hilo, ila taarifa bado hazijathibitisha hilo.
Kundi hiulo limekuwa likishambulia shule katika harakati zake za miaka 5 likitaka kuunda dola ya kiisilamu.BBC

Post a Comment

 
Top