SEHEMU ambayo inasemekana bomu lilitua mara baada ya kutupwa.
Mkurugenzi wa tiba ambaye pia ni kaimu mgamga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo akiongea na waandishi wa habari |
Na Woinde Shizza,Arusha.
Mlipuko
unaosadikiwa ni bomu umelipuka usiku wa kuamkia leo jijini Arusha
katika mgahawa wa Traditional Indian Cusine uliopo pembezoni mwa hotel
ya Gymkana jijini hapa na kujeruhi watu nane.
Akithibitisha
kupokea wagonjwa walioathiriwa na bomu hilo, Mkurugenzi wa tiba ambaye
pia ni kaimu mganga mkuu wa hospitali ya Seliani Dr. Paulo Kisanga
alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 4:30 usiku katika eneo
kwani walianza kupokea wagonjwa hao kuanzia majira ya saa tano kasoro na
saatano .
Alisema
kuwa walipokea wagonjwa nane ambao waliumia sana katika maeneo ya miguu
ambapo alibainisha kuwa katika wagonjwa hao na ne kuna mmoja ambaye
aliletwa akiwa na hali mbaya sana kitu ambacho kiliwalazimu kumfanyia
upasuaji usiku huo huo.
"kati
yawagonjwa hao nane,mmoja alikutwa akiwa mahututi ,kwani mguu wake
ulikuwa umeathiriwa sana na bomu hilo ,ivyo ikatulazimu kumkata mguu
mmoja wa kushoto ,mgonjwa huyo ambaye tumemkata mguu anaitwa Deepak
Gupta (25) mwanaume,na sasa ivi anaendelea vyema kidogo na yupo katika
chumba cha ICU ndani ya hospitali hii yetu ya Seliani"alisema Kisanga
Alisema
kuwa katika majeruhi au nane aliowapokea wanawake wako watatu huku
wanaume wakiwa watano na kubainisha kuwa wote wameshafanyiwa upasuaji na
wapo wodini kwa ajili ya uangalizi wa madaktari
Aidha
aliwataja majeruhi hao kwa majina kuwa ni pamoja na Vinod Suvesh(37),
Ritwik Khandelval (13),Raj Rajin(30),Prateck Saver,manci Gupta(14)
,Manisha Gupta (36),Mahush Gupta(42) pamoja na Deepak Gupta (25) wote
wakiwa na asili ya kiasia.
Kisanga
alisema kuwa kwa mujibu wa wagonjwa hao walio waliofika hapo hospitali
walidai kuwa bomu hilo lilirushwa kwa kupitia dirishani.
Post a Comment