0


Serikali yatangaza nafasi za kazi 1,324.
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma inawatangazia Watanzania wenye sifa na uwezo kujaza jumla ya nafasi wazi za kazi 1,324 ambazo ni kwa ajili ya waajiri mbalimbali Nchini.

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Bw. Xavier Daudi amesema kuwa nafasi 1,334 zimeainishwa bayana kwenye tovuti ya Sekretarieti ya Ajira ambayo ni www.ajira.go.tz ili kuwawezesha wahitimu wote wenye sifa na uwezo kutuma maombi kwa ajili ya kujaza nafasi hizo ajira Serikalini.

"Nadhani ni vizuri zaidi kwa kila muhitimu anayetafuta kazi serikalini kufungua tovuti ya Sekretarieti ya Ajira kuangalia nafasi za kazi zilizotangazwa na pale anapoiona kazi inayoendana na sifa alizonazo kutuma maombi yake ili kuweza kushindanishwa na wengine....maana ajira za Serikali hivi sasa ni za ushindani hivyo inampasa kila anayetaka kupata kazi serikalini kujiandaa vyema ili kujiweka katika nafasi nzuri zaidi ya kuajiriwa katika Utumishi wa Umma" alisema Daudi.

Post a Comment

 
Top