Makachero
wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kumtia mbaroni mmoja wa
washukiwa wa matukio ya tindikali visiwani hapa Alawi Mohammed Silima
(25) mkazi wa Fuoni Melinne nje kidogo ya mji wa Zanzibar.Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta
Mohammed Mhina, amesema mtuhumiwa anahusishwa na tukio la kumwagia
tindikali Sheha wa Shehia ya Tomondo mjini Zanzibar Bw. Mohammed Omar
Saiidi Kidevu kabla ya kutoweka.Inspekta
Mhina amesema, Mtuhumiwa huyo ambaye kwa muda mrefu alikuwa akisakwa na
Polisi kwa kuhusina na tukio hilo, alikamatwa juzi usiku akiwa
mafichoni katika enero Fuoni baada ya taarifa za kiintelijensia kubaini
kuwepo kwake.Bado
Makachero hao wanaendelea kumhoji mtuhumiwa huyo kwa lengo la kuubaini
mtandao mzima wa matukio mbalimbali yakiwemo ya tindikali yaliyotokea
siku za nyuma visiwani humo.
Kukamatwa
kwa mtuhumiwa huyo kunatokana na taarifa za siri za raia wema ambapo
Jeshi la Polisi lilikua likiendelea na upelelezi wa chini kwa chini wa
kumbaini mtuhumiwa na mahali alipojificha.
Baadhi ya wananchi wa Zanzibar wamepongeza kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo na kuliomba Jeshi la Polisi kuendelea na juhudi zake za kuwafsaka watuhumiwa wengine wanaohusika katika matukio menginne kama hayo siku za nyuma viisiwani hapa.
Tukio la kumwagiwa tindikali kwa Sheha huyo, lilitokea majira ya saa 2.45 usiku Mei 22, mwaka jana, wakati Sheha huyo alipokuwa akirudi nyumba akitoka kuchota maji nyumba jirani. na kujeruhiwa vibaya mgongoni, kifuani, sikio na jicho la upande wa kulia.

Post a Comment