tanki la kuhifadhia maji
kibanda maalumu cha mashine
jamii ikiangalia miradi unapoendelea
(Diwani wa kata ya Mbaya bwana Ali kioi)
HATIMAYE
TATIZO LA MAJI KWA WAKAZI WA KIJIJI CHA NAMIHU LAPATIWA UFUMBUZI,katika hatua nyingine ya kupunguza kama siyo kuondoa kabisa kero mbali
mbali zinazoikabili jamii yetu ,wanakijji wa kijiji cha Namihu wilayani
Liwale Mkoani Lindi wamepata neema ya
kujengewa mradi mkubwa wa maji safi na salama kwa njia ya mtandao wa
bomba mradi ambao umefikia hatuwa za mwisho katika ujenzi wake ambapo
hapo jana wameanza kusukuma maji kutoka kwenye chanzo cha maji hayo hadi
kwenye tanki lililojengwa kijijini hapo Namihu.Akiongea na mdau wangu wa makala
hii diwani wa Kata ya Mbaya Mh.Alli N. Kioi alifafanuwa Kuwa mradi huu
kwa sehemu kubwa umejengwa kwa fedha kutoka Benki ya dunia kama mfadhili
ambayo ilitoa jumla ya fadha sh 281,000,000/= ambapo jamii iliweza
kuchangia sh 3,500,000/= na kwamba mradi uliibuliwa katika ngazi ya kijiji
na hatimaye ulifikishwa ngazi ya Halmashauri ya wilaya ambapo pia
ulipata baraka na kuungwa mkono na mbunge wa jimbo la liwale Mh.Faith
Mitambo.Mradi huu umekuja muda muafaka kufuatia tatizo la maji safi na
salama ikiwa ni pamoja na upatikanaji wake kwa ujumla Kuwa mgumu hasa
nyakati za kiangazi ambapo Mara nyingine wanakijiji waliweza hata
kungojelea maji kwenye vyanzo vyake walifafanua wajumbe wa kamati ya
maji ya kijiji hicho ambao walionyesha kuufurahia na kuhaidi kuuendeleza pindi
watakapokabidhiwa rasmi.Aidha Mh Kioi aliendelea kufafanua kuwa mradi
huu ni kati ya mitatu mingine miwili mmoja uko barikiwa na mwingine uko
mpigamiti ambayo pia ipo katika hatua nzuri ya utekelezaji ,mradi huu
wa kijiji cha Namihu unahusisha tenki ambalo linakadiriwa Kuwa na uwezo
wa kuhifadhi maji yasiyopungua lita za ujazo 30,000 kwa wakati mmoja ambapo
litahudumia wakazi wa kijiji hicho wasiopungua1250(kwa mujibu wa takwimu
za mwenyekiti wa seriali ya kijiji).
Post a Comment