Katibu
wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye ameonja chungu ya uamuzi wa
Serikali wa kusitisha mikutano ya hadhara katika mikoa ya Lindi na
Mtwara baada ya kushindwa kufungua mashina ya chama hicho mjini Mtwara.
Nape
ambaye alikuwa mkoani Mtwara kwa ziara ya siku moja, alijikuta akiishia
kuwakabidhi bendera za chama hicho viongozi wa matawi ili
wakazipandishe wenyewe kimyakimya.
Akizungumzia
hatua hiyo, Nape alisema amri hiyo ya kusitisha mikutano imekuwa
kikwazo na inadidimiza demokrasia katika mikoa hiyo, hivyo Serikali
inapaswa kuibadili ili kuruhusu iendelee kufanyika. Mashina ya chama
hicho ambayo yalitarajiwa kufunguliwa mwishoni mwa wiki ni Shapriya,
Coco Beach na Kwajionee.
“Ni
kweli ilikuwa twende kuzindua kwenye maeneo yenu lakini… lipo agizo
ambalo lilitolewa na Serikali kuzuia mikutano katika mikoa hii, kupitia
kwenu ipo haja ya kufungua mikutano ili demokrasia ipanuke zaidi,”
alisema Nape na kuongeza:
“Amri
hii kwa mtazamo wangu inabaka demokrasia, lazima mikutano iruhusiwe
kama hali ni mbaya, kazi ya Serikali ni kulinda huo usalama… nitakwenda
kushauriana nao ili mikutano ifunguliwe, sidhani kama masikio yanaweza
kuzidi kichwa.”
Akizungumzia hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maisha Maganga alisema Serikali haijatengua agizo hilo.
Post a Comment