Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Kambi
Rasmi ya Upinzani Bungeni imesema Wizara ya Maliasili na Utalii
inaongozwa kwa ubabaishaji na ‘mvutano wa kimasilahi’ baina ya waziri na
katibu mkuu, hivyo kukwamisha shughuli za kuendeleza utalii.
Msemaji
wa kambi hiyo (Maliasili na Utalii), Mchungaji Peter Msigwa alitoa kauli
hiyo juzi wakati akisoma maoni kuhusu hotuba ya Makadirio ya Mapato na
Matumizi kwa wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
Alisema
kambi ya upinzani inasikitishwa na mvutano baina ya Waziri Lazaro
Nyalandu na Katibu Mkuu wake, Maimuna Tarishi ambao unaonyesha udhaifu
wa Serikali.
“Hii
inathibitisha kuwa Serikali ni dhaifu kwa kuwa, waziri na katibu mkuu wa
wizara moja wanafanya kazi bila kushirikiana na kila mmoja anaonekana
kumvizia mwenzake hadharani badala ya kukaa kwa pamoja kutekeleza
maazimio ya Bunge,” alisema Msigwa.
Alisema
kitendo cha Waziri Nyalandu kuwasimamisha kazi wakurugenzi wawili,
lakini wakarudishwa na katibu mkuu huku akisema taratibu za kuwafukuza
hazikufuatwa na hii ni dalili kuwa hata yeye (Nyalandu) siyo msafi kwa
kuwa anashindwa hata kujua mipaka yake ya kazi.
Mbali na
mvutano huo, Msigwa alisema maazimio ya Bunge kuhusu matokeo ya
Operesheni Tokomeza Ujangili yanaendelea kupuuzwa na watumishi wenye
tuhuma wakihamishwa vitengo.
“Ngoma
ikivuma sana hupasuka, tena Mungu siku zote hamfichi mnafiki na debe
tupu haliachi kutika (siyo maneno yangu, bali ya wahenga). Siyo mara ya
kwanza kambi ya upinzani kuhoji juu ya usafi wa Lazaro Nyalandu,”
alisema.
Alisema
Waziri Nyalandu alipozungumza katika kikao cha wadau wa ulinzi wa
maliasili Juni mwaka jana mkoani Iringa, aliahidi kuwa majina ya
majangili yakiwamo ya vigogo yangetangazwa hadharani, lakini hadi sasa
hakuna majina yoyote yaliyotangazwa hadharani.
Uteuzi wa Sarakikya
Msigwa
ambaye pia ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema) alizungumzia kitendo cha
Waziri Nyalandu kumteua Paul Sarakikya kukaimu nafasi ya Mkurugenzi wa
Wanyamapori, jambo alilosema ni kinyume na haki za binadamu.
Msemaji
huyo alibainisha kuwa, wakati wote Watanzania wanajiuliza maswali ambayo
hayajapata majibu kuhusu vigezo vilivyotumika kumteua Sarakikya.
“Katika
Operesheni Tokomeza, mtu huyu alikuwa kiongozi wa utekelezaji wa moja
kwa moja na kinachodaiwa ni uvunjifu wa haki za binadamu, inashangaza
kuona mtu huyu tena ndiye ana nafasi ya kukaimu ukurugenzi, lini kawa
msafi?” alihoji Msigwa.
Post a Comment