Jana,
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani akisindikizwa na polisi waliokuwa
na silaha za moto na mabomu ya machozi, huku wafuasi wake wakizuiwa nje
ya uzio wa Mahakama hiyo kwa sababu za kiusalama.PICHA|MAKTABA
Morogoro.
Kiongozi
wa Taasisi ya Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda ameendelea
kusota rumande baada ya kesi yake kuahirishwa kwa mara nyingine kwa kuwa
jalada la kesi yake, halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es
Salaam lilikoitishwa kwa ajili ya mapitio.
Kesi
hiyo iliyofunguliwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mkoa wa
Morogoro mwaka jana, iko mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mary
Moyo na imekuwa ikitajwa kwa zaidi ya miezi sita, huku Sheikh Ponda
akiendelea kusota rumande baada ya kunyimwa dhamana.
Sheikh
Ponda anakabiliwa na mashtaka matatu ambayo ni kutotii amri halali
iliyotolewa na Mahakama ya Kisutu ya kutokutoa maneno yenye kuharibu
imani za dini na kushawishi watu kutenda kosa ambayo anadaiwa kuyatenda
Agosti 10, 2013 jioni katika eneo la Kiwanja cha Ndege, Morogoro.
Jana,
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani akisindikizwa na polisi waliokuwa
na silaha za moto na mabomu ya machozi, huku wafuasi wake wakizuiwa nje
ya uzio wa Mahakama hiyo kwa sababu za kiusalama.
Mara
baada ya kutajwa kwa kesi hiyo, Hakimu Moyo alisema jalada la kesi
hiyo, bado halijarudi kutoka Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, hivyo
kuiahirisha kesi hiyo hadi Mei 26, mwaka huu itakapotajwa tena.
Upande
wa mashtaka uliwasilisha ombi mahakamani hapo kutaka Sheikh Ponda
kuhojiwa na polisi kuhusiana na mashtaka yanayomkabili. Hakimu Moyo
alikubali ombi hilo na kumtaka Sheikh Ponda kuwa na imani na Mahakama
hiyo, akisema itatenda haki kwa mujibu wa sheria na si vinginevyo.
|
Post a Comment