Maalim
Seif akishiriki katika mazishi ya Sheikh wa Ilunga Shekh.Hassan Kapungu
yaliofanyika katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni Dar es Salaam.
akijumuika na Wanancjiji Dar-es-Salaam.
Wananchi
wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika
makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam.
Wananchi
wakishiriki katika mazishi ya Shekh Ilunga Hasaan Kapungu katika
makaburi ya Magomeni Mwinyimkuu jijini Dar-es-Salaam. (Picha na Salmin
Said OMKR)
Na; Hassan Hamad (OMKR).
Makamu
wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad,
amewaongoza maelfu ya waislamu katika mazishi ya sheikh maarufu wa Mkoa
wa Mwanza na mwanaharakati wa dini ya Kiislamu marehemu sheikh Ilunga
Hassan Kapungu.
Sheikh Ilunga amefariki dunia mjini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya Mwinyimkuu Magomeni.
Katika
uhai wake sheikh Ilunga Kapungu alikuwa mwanaharakati ambaye mara
nyingi alikuwa akiendesha mihadhara ya wazi ya dini ya Kiislamu, ambapo
mwishoni mwa mwaka 2013 alikamatwa kwa tuhuma za uchochezi mkoani Tabora
na baadaye kuachiwa huru.
Kwa
mujibu wa taarifa za kimtandao, kabla ya kukamatwa kwake na kuachiwa
huru Disemba mwaka 2013, marehemu sheikh Ilunga alikwenda nchini India
kwa matibabu baada ya kusumbuliwa na matatizo ya figo pamoja na sukari.
Akizungumza
katika mazishi hayo sheikh Basaleh wa Dar es Salaam, amesema marehemu
sheikh Ilunga alikuwa mwanaharakati imara na ni mfano mzuri wa kuigwa
katika harakati za dini ya Kiislamu.
Mazishi
yake yameweka historia baada ya maelfu ya waislamu kujitokeza kushiriki
kwao, hali iliyopelekea mchanga wa kaburi lake kufukiwa kwa mikono
badala ya kutumia mapauro na majembe kama ilivyozoeleka.
Masheikh kutoka Mikoa mbali mbali ya Tanzania wameshiriki mazishi hayo akiwemo sheikh Kishki.
Post a Comment