Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwasilisha makadirio ya matumizi ya Ofisi yake na
Ofisi ya Bunge kwa mwaka wa fedha 2014/15, wakati wa kikao cha Bunge
mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Dodoma.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda jana aliwasilisha bungeni, bajeti ya ofisi yake na
mfuko wa Bunge inayofikia Sh5.21 trilioni. Kati ya hizo, Sh5 bilioni
zimetengwa kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa
kufanyika baadaye mwaka huu.
Hayo
yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu
(Tamisemi), Hawa Ghasia wakati wa maelezo kuhusu kazi zilizotekelezwa
mwaka 2013/2014 na mwelekeo wa kazi zitakazotekelezwa 2014/2015.
Ghasia
alisema shughuli zitakazogharimiwa na fedha hizo ni pamoja na
maandalizi ya masanduku ya kupigia kura, kupitia kanuni za uchaguzi na
kuandaa fomu na nyaraka mbalimbali za uchaguzi.
|
Post a Comment