Mkutano wa hadhara uliofanyika jana katika shule ya msingi Kipule Magereza.
Mkuu wa wilaya ya Liwale bwana Ephraim Mmbaga na akiwa ameambatana na kamati yake ya ulinzi na usalama,kaimu Mkurugezi wa (w) ya Liwale na waheshimiwa Madiwani na Afisa Elimu wa (W) na watumishi wengine upande wa idara ya Elimu.Mkuu wa wilaya pamoja na timu hiyo jana aliafanya mkutano wa hadhara na wananchi katika shule ya msingi Kipule Magereza.Lengo la ziara hiyo ni kuongelea swala zima la vitendo vinavyohusishwa na imani za kishirikina vinavyofanywa na wananchi wa kijijini hapo kuwafanyia Walimu wa shule ya msingi kipule magereza.Walimu wa shule hiyo wamedai kutishwa na vituko vya ajabu usiku wa manane na kupelekea walimu hao kutokuwa na imani ya kufundisha katika shule hiyo hali ambayo itapelekea kurudisha nyuma jitihada za serikali katika kuipa jamii huduma ya Elimu. Moja ya vituko kama kusikia sauti za watu wengi wakiongea nje ya uwa wakitoka nje kuangalia huwa hawaoni watu.
Mkuu wa wilaya na timu yake wamewasa wananchi kuacha vitendo hivyo vya kuwatisha walimu na kuwataka kushirikiana nao vizuri ili watoto wao wapate elimu bora na akaongeza kusema kama vitisho vitajirudia tena itapelekea shule hiyo kufungwa na Walimu kuhamishwa kwa ajili ya usalama wao.
Wananchi na Wazee wa kijiji hicho alitoa tamko na kumwahidi DC kuwa swala hilo halitajirudia tena.
Post a Comment