Ni
picha ambayo nimetumiwa na Mwandishi wa habari wa Kenya ikimuonyesha
Uhuru Kenyatta ambae ni Rais wa nchi hiyo akiwa na naibu wake William
Ruto baada ya kuamua kusimama njiani wakitokea Arusha kwa gari na kula
chakula chini ya mti Kajiado.Rais Uhuru ameripotiwa kufanya mambo kadhaa
ambayo hayajawahi kufanywa na Marais wengine wa nchi hiyo likiwemo la
kutembea Nairobi bila msafara ambapo hivi juzi kuna video ilitoka
ikidaiwa kumuonyesha Rais huyo akinunua karanga kutoka kwa watoto
barabarani Nairobi.Hii picha ya leo hapo juu inadaiwa ni msafara wake
uliosimama na kula chakula wakati akitokea Arusha Tanzania kwenye
mkutano ambapo alitumia usafiri wa gharama nafuu (gari) na kuendeshwa
kutoka Nairobi, siku kadhaa tu baada ya nchi hiyo kutangaza kuvunja
safari za nje ya nchi za viongozi wa serikali zisizo za lazima ili
kuokoa matumizi makubwa ya fedha.
Ni siku
kadhaa pia baada ya Rais huyu kutangaza maamuzi ya kupunguza mshahara
wake, naibu wake, Mawaziri na hata wakuu wa mashirika ya umma nchini
humo.
picha ya lunch imepigwa na Rebecca Nduku hii ya chini ni Capital fm Kenya.
Post a Comment