0



Na Ahmad Mmow, Lindi.

WANANCHI wa kijiji cha Kichonda, wilaya ya Liwale, mkoa wa Lindi, licha ya kumhakikishia naibu waziri wa ardhi,Angelina Mabula(Mb), kuwa wapotayari kuwapokea wawekezaji watakao kwenda kuwekeza katika kijiji hicho.Lakini hawamtaki mwekezaji aliyekwenda na kuomba ardhi kwa ajili ya  kilimo cha mazao mseto.

Hayo yalijiri juzi kijijini hapo wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na naibu waziri huyo, ambao pamoja na mambo ulitumika kuwaelewesha wananchi hao umuhimu na faida za kuhaulisha ardhi kwa maendeleo yao na taifa.

Walisema kwakipindi kifupi ambacho wamekuwa nae mwekezaji huyo ambae kwasasa jina lake linahifadhiwa kwasababu ya maadili ya uandishi, ameonesha kutokuwa mwaminifu.
Hasa katika kuteleza makubaliano na masharti ya awali ambayo alipewa.Ikiwamo ahadi aliyotoa mwenyewe ya kuchimba kisima kwa ajili ya maji safi na salama.
Mmoja wa wananchi hao,Rashid Mnyupe  alisema  katika kipindi kifupi ambacho wamekuwa na mwekezaji huyo wamebaini kuwa ni muongo.

Hivyo sio muaminifu na hafai kupewa ardhi kwa ajili ya uwekezaji anaokusudia kufanya katika kijiji hicho.Ikiwamo kushindwa kutekeleza makubaliano ya awali.
"Alihaidi angeleta maji safi na salama,lakini hajafanya hivyo.Kwahiyo hatutaki apewe ardhi na mchakato wa kumpa usitishwe Kwasababu mapema tu ameonesha kukosa uaminifu,"alisisitiza Mnyupe.

Kauli ya Mnyupe iliungwa mkono na mwananchi mwingine aliyejitambulisha kwa jina la Sofia Kilola,ambae nae alisma wananchi hawakatai wawekezaji na wanawakaribisha kwenda katika kijiji hicho kuwekeza katika miradi mbalimbali. 

Ikiwamo kwenye ardhi kwa ajili ya kilimo Hata hivyo mwekezaji aliyejitokeza kwa ajili ya kilimo mseto hatoshi na hafai kupewa ardhi kijiji hapo.
"Kutenga ardhi na kuhaulisha tupotayari,lakini sio kwa mwekezaji huyu ambae mapema tu ameonesha kukosa uaminifu Zoezi la kumpa ardhi lisimame,"Sofia alipigilia msumari maneno ya Mnyupe.

Kwaupende wake,waziri Mabula licha ya kuhimiza wananchi hao wahaulishe ardhi kwaajili ya maendeleo yao na taifa kwa kwamjula Alisema hawezi kuwalazimisha wamkubali mwekezaji wasie mhiataji Bali wahaulishe na kuwapokea wawekezaji wanaotaka kuwekeza kwa ajili ya maendeleo yao na taifa.

Waziri Mabula amehitimisha ziara yake mkoani humu.Ambapo alizungumza na wananchi,viongozi na watendaji katika wilaya za Nachingwea na Liwale

Post a Comment

 
Top