0
Mafia ,TanzaniaHaki miliki ya pichaGOOGLE
Image captionAjali ya boti yatokea kisiwani Mafia, watu sita wahofiwa kufa
Watu sita wanahofiwa kufa maji baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka bahari, karibu na Kisiwa cha Mafia Tanzania,kutokana na dhoruba kali.Mbunge wa jimbo la Mafia, mkoani Pwani Mbaraka Dau amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Mwishoni mwa wiki hii ilitokea ajali ya boti iliyosababisha watu sita , miongoni mwao raia sita wa Tanzania na mmoja mwenye asili ya Marekani , waliokuwa wakisafiri kutoka katika bandari ya Nyamisati iliyoko wilaya ya Kibiti mkoa wa pwani , wakielekea katika pwani ya Kilindoni iliyoko katika wialaya ya Mafia katika shughuli za kimishionari (masuala ya dini ya Kikristo) .
Anaeleza Mbunge wa Mafia Mbaraka Dau, kuwa walipofika kati kati ya Mafia na Nyamisati kulitokea dhoruba na kusababisha chombo chao kupinduka abiria wote sina wakatumbukia baharini na kusambaratika , siku ya Ijumaa tarehe nne mwezi huu .
Nahodha wa chombo hicho ni yeye pekee aliyenusurika na hivyo kuogelea mpaka katika kijiji cha jirani kilichopo Wilaya ya Mkuraranga kisiwa cha Koma, na kuwasili Ijumaa tarehe nne, majira ya asubuhi ili kupata huduma ya kwanza katika zahanati ya Koma na kisha baadaye kuhamishiwa katika hospitali ya Kimishionari ya Kisiju na kulala kwa usiku mmoja na jana na kuhamishiwa katika hospitali ya Agakhan, Mjini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mbunge wa Mafia Ramadhani Dau, anaeleza kuwa watu watano waliokuwa wameabiri chombo hicho akiwemo raia mmoja wa Marekani ambaye jina lake ni Kennethi bila kujua jina lapili anaarifu kuwa wote hawajapatikana mpaka sasa na juhudi za kuwasaka zinaendelea tangu juzi huku boti mbili za hifadhi ya bahari za kisiwa cha Mafia, zikitokea kisiwani humo zilitia nanga Kisiju na kumchukua nahodha aliyenusurika na kumpeleka katika bandari uya Kisiju.
Siku ya jana boti hizo zikisaidiana na chopa ya jeshi la polisi zilisaidiana kufanya doria, ili kubaini kama kuna miili yoyote inayoelea baharini bila ya mafanikio yoyote, na zoezi linaendelea tena hii leo doria inaendelea katika Kisiwa cha Koma na Kwale , katika eneo la Kisiju .
Kutokana na uzoefu wa nyakati za hali ya hewa, wakati huu ni msimu wa pepo za Kusi , hivyo maiti hizo huenda zikaonekana Dar es Salaam ama Zanzibar ,bandari za Kuruti,Kisiju, bandari ya Buza na kisiwa cha Sukuti na maeneo yote yenye mikoko ndiyo maeneo yanayotiliwa zaidi mkazo katika juhudi za kuwatafuta watu hao.

Post a Comment

 
Top