0
Kim Jong-un (L) talking with South Korea's President Moon Jae-in (R) before the inter-Korean summit at the Peace House building on the southern side of the truce village of Panmunjom on 27 April (picture released by North Korean state media)Haki miliki ya pichaAFP PHOTO/KCNA VIA KNS
Image captionKim Jong-un na rais wa Korea Kusini Moon (kulia) walikutana kwa mazungumzo ya kihistoria tarehe 27 Aprili
Rais wa Marekani Donald Trump ametoa matamshi yanayokinzana na ya mshauri wake wa kitaiafa kuhusu usalama, akisema mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia hauwezi kutumiwa nchini Korea Kaskazini.
Pendekezo la John Bolton liliigadhabisha Korea Kaskazini ambayo ilitisha kujitoa kwa mkutano na Trump wa mwezi ujao.
Bw Trump alisema anaamini mkutano huo utafanyika.
Mwaka 2003 kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi alikubali kuachana na mpango wake ya nyuklia ili apate kuondolewa vikwazo.
A US Air Force F-22 Raptor lands at Gwangju airbase, South Korea, 16 May 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNdege ya jeshi la Marekani ikitua uwanja wa Gwangju nchini Korea Kusini 16 Mei 2018
Hata hivyo aliauwa na waasi walioungwa mkono na nchi za magharibi miaka kadhaa baadaye, mfano amabao ulionekana kumtia wasi wasi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un.
Pyongyang ilionya Jumatano kuwa huenda isihudhurie mazungumzo ambayo yanapangwa kufanyika nchini Singapore tarehe 12 mwezi Juni.

Rais Trump alisema nini?

Huku Bolton akitazama, Rais Trump alisema: Mfumo wa Libya si mfumo tuko nao kabisa wakati tunafikiri kuhusu Korea Kaskazini.
Makubaliano ambayo Bw Trump alikuwa akizungumzia na Kim Jong-un ni kitu ambacho Kim atakuwepo, atakuwa nchini mwake, ataiongoza nchi yake na nchi yake itakuwa tajiri sana.
"Ukiangalia Korea Kusini, huu utakuwa mfumo sawa na wa Korea Kusini kimaendeleo.. ni watu wanaojitahidi sana."
Kuhusu mkutano uliopangwa, Trump alisema: Hakuna kilichobadilika na Korea Kaskazini tunachokifahamau, hatujaambiwa chochote
John Bolton, national security adviser, listens as President Trump speaks during a meeting in the Oval Office of the White House May 17, 2018Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionJohn Bolton alitazama huku Trump akiweka wazi hisia zake

Korea Kaskani inaonaje suala hili?

Pia Alhamisi, Korea Kaskazini ilisema haitarejea kwenye mazungumzo na Korea Kusini hadi pale masuala tata kati yao yatasuluhushwa.
Pyongyang imegadhabishwa na kuendelea kwa mazoezi ya pamoja ya kijeshi kati ya Marekani na Korea Kusini ambayo inayaona kama matayarisho ya uvamizi. Ilifuta mazungumzo ya juu na Korea Kusini mapema wiki hii.
Kwenye taarifa mpatanishi mkuu Ri Son-gwon alikosoa mamlaka za Korea kasini kwa kukosa uangalifu kufuatia hatua ya kumruhusu raia wa Korea Kaskazini aliyekimbilia Korea Kusini kuzungumza kwenye bunge mjini Seol.
A US Air Force F-22 Raptor lands at Gwangju Air Base in the south-western city of Gwangju, S Korea, on May 16, 2018Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMazoezi ya pamoja kati ya Marekan na Korea Kusini yameigadhabisha Korea Kaskazini
Korea Kaskazini inaonekana kuweka shinikizo kwa Marekani na Korea Kusini na kukataa mazungumzo hadi matakwa fulani yatimizwe.

Ni kwa nini mfumo wa Libya unazungumziwa?

Tangazo la Korea Kaskazinia kuwa huenda ikajitoa kwa mkutano na Marekani lilinyooshea kidole mshauri wa usalama wa Marekani John Bolton.
"Hatukuficha hisia zetu dhidi yake," ilisema tarifa ya Jumatano, ambayo iliandikwa na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni Kim Kye-gwan.
Korea Kaskazini ilikuwa ikimaanisha mahojiano ya Bolton akiufananisha na mfumo wa Libya wa kumaliza zana za nyuklia
Mwaka 2003 Kanali Muammar Gaddafi alikubali kuachana na programmu ya silaha za maangamizi makubwa kwenye tangazoa lililoishangaza dunia.
Vikwazo vingi vya Marekani dhidi ya Libya viliondolewa ndani ya miezi michache na uhusiano wa kidiplomasia ukarejeshwa.
Lakini mwaka 2011 Gaddhafi alipinduliwa na waasi wakiungwa mkono na Nato. Baadaye alikamatwa na kuuawa na vikosi vya waasi.

Post a Comment

 
Top