0

Tanzania ina upungufu wa wataalam 8725 wa ugani katika sekta ya kilimo na mifugo hali inayofanya kuendelea kuwepo kwa kilimo na ufugaji usio na tija.

Hayo yameelezwa na Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha maadhimisho ya siku ya wakulima ambayo sherehe zake zimefanyika katika viwanja vya Ngongo, Mjini Lindi

Mhe. Samia amesema serikali imeendelea na jitihada za kuongeza wataalam wa kilimo na mifugo kupitia wakala wake wa vyuo vya elimu ya kilimo na mifugo, na kufanikiwa kuongeza wataalam wa mifugo kutoka 2,451 mwaka 2014/2015 hadi kufikia wataalam 2,500 ambapo kati yao 1,034 ni wa Stashahada na 1,466 ni wahitimu wa Astashahada.

Pia Mhe. Samia mwezi Juni mwaka huu vyuo hivyo vimetoa wahitimu 1,471 na kufanya idadi ya wataalam nchini kufikia 8,600 kati ya wataalam 17,325 wanaohitajika.

Post a Comment

Emoticon
:) :)) ;(( :-) =)) ;( ;-( :d :-d @-) :p :o :>) (o) [-( :-? (p) :-s (m) 8-) :-t :-b b-( :-# =p~ $-) (b) (f) x-) (k) (h) (c) cheer
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.

 
Top