Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAtletico Madrid wameshinda Europa League mara tatu, ambapo wanashikilia rekodi sasa na Sevilla
Antoine Griezmann alifunga mabao mawili na kuwawezesha Atletico Madrid kuwachapa Marseille 3-0 mjini Lyon, Ufaransa na kushinda Kombe la Europa League mara yao ya tatu katika kipindi cha miaka tisa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa alianza kwa kufunga baada ya Andre Zambo Anguissa kutomakinika na mpira dakika ya 21 na kisha akafunga la pili dakika ya 49.
Nahodha wao Gabi alifunga bao la tatu dakika ya 89 na kuwawezesha vijana hao wa Madrid kushinda kombe hilo ambalo pia walilitwaa miaka 2010 na 2012.
Matokeo yangelikuwa tofauti iwapo mshambuliaji wa Marseille Valere Germain angetumia nafasi yake mapema kwenye mechi kabla ya Griezmann kufunga.
Nahodha wa Marseille Dimitri Payet aliondoka uwanjani akichechemea kutokana na jeraha baada ya kukaa uwanjani nusu saa pekee, na sasa huenda akakosa kushiriki Kombe la Dunia.
Bila kiungo huo wao, Wafaransa hao waliwatishia Atletico mara moja pekee, mshambuliaji wa zamani wa Fulham Kostas Mitroglou alipogonga mlingoti wa goli kwa mpira wa kichwa.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAntoine Griezmann amewafungia Atletico Madrid mabao 30 msimu huu
Atletico wamekuwa moja ya klabu ambazo zimekuwa zikifanya vyema sana Ulaya miaka ya karibuni.
Walifanikiwa kuzima ubabe wa Barcelona na Real Madrid La Liga kwa kushinda ligi 2013-14.
Kwa sasa wanashikilia nafasi ya pili ligi kuu Uhispania wakiwa wamesalia na mechi moja na wamo mbioni kumaliza katika tatu bora kwa msimu wa sita mfululizo.
Katika kipindi hicho, wamefika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili, ambapo walishindwa na wapinzani wao wa jiji Real Madrid.
Meneja wao Diego Simeone alitazama mchezo huo kama shabiki kwani anatumikia marufuku ya mechi nne baada ya kuadhibiwa wakati wa mechi kati ya nusufainali kati ya Arsenal na Atletico.
"Nina furaha sana," alisema Griezmann baada ya mechi.
"Nimekuwa nikitia bidii kwa sababu ya tukio hili kwa miaka mingi. Niliondoka nyumbani nilipokuwa na miaka 14 juu ya hili. Tutasherehekea. Familia yangu iko hapa."
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMashabiki wa Marseille waliondoka Lyon kwa masikitikoHaki miliki ya pichaREX FEATURESImage captionGriezmann akisherehekea
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionAliyekuwa beki wa zamani wa klabu ya Real Madrid fernando Hierro
Aliyekuwa beki wa Real Madrid Fernando ...Read more »
Image captionMwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremayew Anas akihojiwa na wanahabari kuhusu makala yake ya upelelezi yaliochukua miaka miwili
Takriba...Read more »
Haki miliki ya pichaSPORTPESA
Mabingwa wa ligi ya Tanzania bara Simba wametinga fainali ya michuano ya Super Cup ya kampuni ya Sportspesa baada ya ku...Read more »
Image captionAliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc
Chelsea inakaribia kumsajili aliyekuwa kocha wa Ufaransa na PSG Laurent Blanc kuchukua ...Read more »
Mwanamasumbwi wa Marekani Floyd Mayweather ametetea taji lake katika porodha ya Forbes ya wanamichezo wanaopata mapato ya juu zaidi duniani.
...Read more »
Mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane, 26, alikubali kujiunga na Real Madrid kabla ya Zinedine Zidane kujiuzulu kama kocha wa mabingwa hao...Read more »
Post a Comment
aprieztmkrdezign
218168578325095
Emoticon
Click to see the code! To insert emoticon you must added at least one space before the code.
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.