0
Jose Mourinho
Image captionJose Mourinho
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wa kati wa Brazil Fred kutoka klabu ya Shakhtar Donetsk ili kuchukua mahala pake Paul Pogba. Manchester City pia inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21.. (Mirror)
Real Madrid inataka kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Pogba lakini rais Florentino Perez anasema kuwa hawezi kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hadi pale atakapopunguza mshahara wake na kuonyesha mchezo mzuri wakati wa kombe la dunia nchini Urusi. (Express)
Kylian Mbappe
Image captionKylian Mbappe
Manchester City Inalenga kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa na PSG Kyllian Mbappe, 19, na kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara katika uwanja wa Etihad mwisho wa msimu huu (Sky Sports)
Kiungo wa kati wa Norwich City na Uingereza James Maddison, 21, anasakwa na vilabu kadhaa katika ligi ya Premia ikiwemo Tottenham, Arsenal, Everton na Manchester City. (Telegraph)
Borussia Dortmund inataka kumsajili Michy Batshuayi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Chelsea
Image captionBorussia Dortmund inataka kumsajili Michy Batshuayi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Chelsea
Borussia Dortmund inataka kumsajili Michy Batshuayi, ambaye yuko kwa mkopo kutoka Chelsea, kwa kandarasi ya kudumu mwisho wa msimu huu.Chelsea inataka zaidi ya £50m ili kumuuza mchezaji huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 24. (Evening Standard)
Chelsea inataka kumsajili kiungo wa kati wa Nice Jean Michael Seri kwa dau la £35m, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Ivory Coast anatarajiwa kusubiri na kuona ni nani mkufunzi wa Blues msimu ujao. (Mirror)
Beki wa kushoto Luke Shaw hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu ya Manchester United
Image captionBeki wa kushoto Luke Shaw hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu ya Manchester United
Beki wa kushoto Luke Shaw hajaamua kuhusu hatma yake katika klabu ya Manchester United . Mchzaji huyo mwenye umri wa miaka 22 ataamua mwishoni mwa msimu huu, baada ya kuwa na uusiano mbaya na Mourinho.. (ESPN)
Barcelona imetenga kitita cha £60m ili kumsajili mshambuliaji wa Manchester United na Ufaransa Anthony Martial, 22, huku mchezaji wa Fulham Ryan Sessegnon, 17,pia akiripopotiwa kusakwa na klabu hiyo.. (Mail)
Winga wa Benfica na Serbia Andrija ZivkovicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWinga wa Benfica na Serbia Andrija Zivkovic
Liverpool na Tottenham walikuwa miongoni mwa klabu nyingi za ligi ya Uingereza kutuma maskauti wake kumtazama winga wa Benfica na Serbia Andrija Zivkovic siku ya Jumapili katika mechi na Porto. (Sun)
Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anaamini dirisha fupi la mwisho wa msimu litatoa fursa kwa Tottenham kuanza vizuri katika ligi ya Uingereza. (ESPN)
Huddersfield itampatia meneja wake David Wagner kandarasi mpya ya miaka miwili na mshara mpya Mkufunzi huyo alikuwa amehusishwa na uhamisho wa kurudi klabu ya Borussia Dortmund. (Sun via Huddersfield Examiner)
Beki wa Manchester United, 28, Matteo Darmian kulia
Image captionBeki wa Manchester United, 28, Matteo Darmian kulia
Southampton inataka kumsajili kipa wa Sheffield Wednesday Keiren Westwood, 33, kuchukua mahala pake Fraser Forster, 30, ambaye yuko tayari kuondoka klabuhiyo ya watakatifu mwisho wa msimu huu.Celtic na Leeds pia wameripotiwa kumtaka mchezaji wa Ireland kaskazini Westwood. (Sun)
Fulham itampatia mkufunzi mkuu Slavisa Jokanovic mpango mpya lakini atasubiri hadi mwisho wa msimu ili kufanya hivyo.. (Evening Standard)
Beki wa Manchester United, 28, Matteo Darmian anasema kuwa anatamani kuelekea Itali na kwamba amefurahi kwamba Juventus wanamtaka (Sky Sports Italia)Kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish ananyatiwa na klabu ya Leicester City, huku mchezaji huyo mweny umri wa miaka 22 akisubiriwa kuondoka Villa Park iwapo klabu hiyo itafeli kupanda daraja hadi katika ligi ya Premia . (Mirror)

Post a Comment

 
Top