0
Afisa Maendeleo wa Mkoa Rukwa akitoa elimu ya namna ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi wa shule saba za mjini Sumbawanga mapema leo mjini humo. Kampeini ya Kutokomeza mimba na ndoa za utotoni inatolewa Wizara ya Afya(Maendeleo ya Jamii). Picha zote na Wizara ya Afya. 
Afisa Maendeleo Jamii Mkuu wa Wizara ya Afya Bw. Christopher Mushi akitoa elimu ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi kutoka shule saba za mji wa Sumbawanga leo mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa. 
Wanafunzi kutoka shule saba za Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa wakifuatilia kwa makini kampeini ya kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mapema leo kufuatia juhudi za Wizara ya Afya(Maendeleo ya Jamii) kutokomeza mimba na ndoa za utotoni hapa Nchini. 
Madereva bodaboda wa mji wa Sumbawanga wakiwasili Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Rukwa kushiriki kampeini za kutokomeza mimba na ndoa za utotoni mapema leo mjini sumbawanga. 



Na Anthony Ishengoma-Wizara ya Afya. 

Mkoa wa Rukwa kwasasa huna jumla ya kesi 256 zinazohusiana na mimba kwa wanafunzi wa kike wa shule za sekondari na Msingi. 

Akiongea katika Mkutano uliondaliwa na Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii na Ofisi ya Mkoa wa Rukwa kwa madereva bodaboda kuhusu mimba na ndoa za utotoni Kaimu KatibuTawala Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Bw. Abubakari Kunenge amesema idadi ya kesi hizi imepatikana kwa kipindi cha miezi tisa kwa mwaka 2017/18. 

Aidha Bw. Kunenge amesema kuwa kwa baadhi ya baba wa familia mkoani Rukwa wanadhani wanadhani mimba za utotoni sio tatizo na linafanyika bila kujali madhara yake. ”Suala la mimba za utotoni ni suala la kosa kisheria na ukosefu wa haki ya mtoto ambalo lazima tulikomeshe Mkoani kwetu”.Alisisitiza Bw. Kunenge. 

Kaimu Katibu tawala huyo pia amesema tatizo la mimba na ndoa za utotoni ni kikwazo kwa juhudi za serikali la kuwa na uwakilishi wa 50/50 katika nafasi mbalimbali za uongozi. Ameongeza kuwa suala la Mimba za utotoni pia linachangia ongezeko la watoto wa mitaani akiutaja mkoa wake kuwa pia uko juu kitakwimu kwa kuwa na idadi kubwa ya watoto wa mitaani. 

Aidha Dereva boda boda Mkoani Rukwa Bw. Ezekia Kalinga akichangia mjadala wa mimba na za utotoni amesema mazingira ya kusomea wanafunzi sio mazuri kwa sababu baadhi ya mabinti wanasafili umbali mrefu kutoka nyumbani hadi shuleni. Aidha Bw. Kalinga amesema wanafunzi wasiokuwa wavumilivu kwasababu tu ya ukosefu wa chakula shuleni mwanafunzi anajikuta amejiingiza katika matendo yasiyofaa. 

Kwa mjibu wa takwimu za jeshi la polisi mkoani Rukwa Wilaya ya Nkasi inaoongoza kwa kuwa na wanafunzi 106 ikifuatiwa na Wilaya za Sumbawanga vijijini 58,Sumbawanga mjini 56 na Wilaya ya Kalambo ni wanafunzi 36.

Post a Comment

 
Top