0
Wakimbizi wa Burundi
Image captionWakimbizi wa Burundi
Serikali ya Tanzania inasema kuwa inajiondoa katika mpango wa Umoja wa mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.
Tanzania limekuwa eneo salama kwa wakimbizi wengi na sasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 wa Burundi ambao walitoroka mzozo.
Rais John Pombe Magufuli amesema kwamba taifa lake linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na lile la kifedha .
Makataa ya wakimbizi wa Burundi kuondoka Tanzania yakamilika
Mwaka uliopita taifa hilo lilisimamisha kwa muda usajili wa wakimbizi wapya na kuwataka wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani , hatua ambayo ilishtumiwa na makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.
Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa kinasema kuwa kinatuma ujumbe wa ngazi za juu kwa mazungumzo na serikali ya Tanzania.
Tanzania ndio nchi inayohifadhi wakimbizi wengi zaidi kutoka Burundi kuliko nchi nyingine yoyote ile katika ukanda wa Afrika Mashariki.
hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Image captionhadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya shirika la wakimbi la Umoja wa Mataifa UNHCR.
Ripoti hiyo anasema hadi hivi sasa, kuna wakimbizi Laki 2 na elfu 41 kutoka Burundi wanaopatiwa makazi nchini Tanzania.
Katika idadi hii kubwa ya watu wanaokimbia nchi yao, UNHCR inasema asilimia 60 ni watoto.
Na ndani ya kipindi cha miezi mitano tu ya mwaka huu wa 2017, wakimbizi 44,487 wamekimbia Burundi na kuingia Tanzania
UNHCR inasema huu ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchii hii haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu, ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000
Image captionKambi moja kwa mfano ya Nyarugusu, ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000
Kambi moja kwa mfano ya Nyarugusu, ambayo inatajwa kuwa ni moja ya kambi kubwa za wakimbizi duniani, inahifadhi wakimbizi 139,0000 idadi ambayo inapaswa kupunguzwa na kuwagawa wakimbizi katika kambi nyingine.
Lakini hili limeshindikana, ripoti ya UNHCR inasema, na ni kwasababu ya kukosekana kwa ardhi ya kufungua kambi mpya.BBC

Post a Comment

 
Top