Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ametangaza baraza lake jipya la mawaziri.
Waziri wa zamani wa fedha Nhlanhla Nene amerejeshwa tena katika nafasi hiyo.
Nene alifukuzwa Disemba 2015 na Rais wa zamani Jacob Zuma na nafasi yake ikachukuliwa na Des van Rooyen.
Palipotokea anguko la thamani ya randi alilazimika kumfukuza Rooyen na kumchagua Pravin Gordhan, siku nne baadae ambaye pia alimfukuza kazi siku za mbeleni.
Katika baraza la Ramaphosa, Gordhan amerejea kama waziri wa masuala la biashara.
Post a Comment