0
Olivier Giroud
Image captionOlivier Giroud
Chelsea imemsajili mshambuliji wa Arsenal Olivier Giroud kwa mkataba wa miezi 18 utakaogharimu £18m.
Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31, anaondoka arsenal baada ya kufunga maba 105 katika mechi 253 tangu asajiliwe kutoka klabu ya Ufaransa ya Montpellier kwa kitita cha £12m mnamo mwezi Juni 2012.
Borussia Dortmundpia wamethibitisha kumsajili mshambuliaji wa Chelsea Michy Batshuayi hadi mwisho wa msimu huu.
Awali Dortmund ilimuuza Pierre-Emerick Aubameyang kwa Arsenal.
Riyad Mahrez
Image captionRiyad Mahrez
Wakati huohuo Manchester City wamejiondoa katika makubaliano ya kumsajili winga wa Leicester Riyad Mahrez wakidai kwamba uhamisho wake ungeigharimu klabu hiyo dau kubwa la £95m.
Siku ya Jumanne mchezaji huyo alikuwa amewasilisha ombi la kuondoka katika klabu yake ya Leicester

Post a Comment

 
Top