0
Picha inayohusiana
Timu ya Soka ya Tanzania kwa upande wa wanawake imepanda nafasi sita katika ubora wa kandanda Ulimwengu katika viwango vilivyotolewa Disemba 15 na Shirikisho la Soka Duniani 'FIFA'.

Tanzania imepata alama 960 ambazo ni sawa na alama zilizopita lakini imefanikiwa kukwea hadi nafasi ya 102 kutoka nafasi ya 108 iliyokuwa hapo awali.

Kwa nafasi hiyo Tanzania imeendelea kuongoza kwa upande wa nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, wakifuatiwa na Rwanda Waliokuwa kwenye nafasi ya 105, huku Kenya wakiwa nafasi ya 108, Uganda wapo nafasi ya 111 na Burundi ndio wa mwisho.

Katika kipindi hiki timu ya Tanzania chini ya umri wa miaka 20 ilicheza michezo ya kuwania kombe la dunia ambayo ilitolewa kwa jumla ya mabao 9-0 na timu ya soka ya Nigeria ambao bado wanaongoza Kwa upande wa Afrika wakiwa nafasi ya 37 duniani.
Marekani. 
Ulimwenguni Marekani wameendelea kuongoza wakifuatiwa na Ujerumani waliokuwa nafasi ya pili na nafasi ya tatu bado inashikiliwa na England.

Post a Comment

 
Top