0

,,Kuna mwalimu wa shule moja ya sekondari alikuwa amezoea kumchapa viboko
mwanafunzi mmoja mchelewaji.

Mwanafunzi huyu alikuwa akichelewa kipindi cha kwanza
kila siku. Hivyo, siku ambazo mwalimu huyu alikuwa na kipindi cha kwanza, mwanafunzi
huyu alikuwa anachapwa kwanza kabla ya kuingia darasani. Hali hii iliendelea kwa muda
mrefu. Wiki moja ilipita bila yule mwanafunzi kuonekana shuleni.
Wiki lililofuata yule mwanafunzi alifika shuleni mapema sana kabla ya mwanafunzi
mwingine yeyote. Mwalimu yule alipomwona alifurahi sana. Alipoingia darasani alimwita
yule mwanafunzi na kumsifia sana mbele ya darasa.

"Radhia, simama. Darasa, Mpigieni makofi "Radhia" kwa sababu leo kawa wa kwanza kufika
shuleni. Kumbe fimbo zile zimesaidia enhe"
Wanafunzi walipiga makofi huku wengine wakimcheka huyo "Radhia". Baada ya wanafunzi
kumcheka na kumfanyia dhihaka Radhia alimwomba mwalimu ampe nafasi aseme jambo.

Mwalimu akamruhusu.
Kwa sauti ya upole akasema, "Mwalimu, siku zote nilizokuwa nikichelewa kufika shule
nilikuwa namuuguza mama yangu. Baba yangu alifariki kabla sijazaliwa. Nimelelewa na
mama yangu tu. Simjui ndugu yeyote. Mama yangu alipokumbwa na maradhi alipelekwa
hospitalini lakini maradhi yake hayakuonekana. Akaruhusiwa kurudi nyumbani akiwa na
dawa za kutuliza maumivu tu. Kwa sababu hatuna pesa, hakuweza kupelekwa popote
kwa vipimo zaidi."
Radhia alifuta machozi yaliyoanza kutiririka mashavuni, akamtizama Mwalimu wake kusha
akaendelea;
"Hivyo kwa kipindi chote nilichokua namuuguza mama, nilitakiwa kufanya usafi wa
nyumba, kuchota maji, kumsafisha mama yangu, kumwandalia chakula chake kabla ya
kuja shuleni."
Radhia alinyamaza kidogo kisha akaendelea; "Lakini leo nimewahi kwa sababu mama
yangu alifariki wiki iliyopita. Kwa hiyo kilichokuwa kinanichelewesha kimeondoka ndo
maana leo nimewahi shuleni."
Baada ya hapo Radhia hakuweza kuongea tena. Taratibu akakaa kitini huku akilia kwa
kwikwi. Darasa zima liligeuka mahala pa msiba na simanzi kuu.

FUNZO: Usimhukumu mtu bila kumpa nafasi ya kumsikiliza. Kama ime kugusa isamabaze kwa kushare na kwa wenzetu wengine wapate kujifunza...
Share kama umeguswa

Post a Comment

 
Top