0
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Image captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Korea Kaskazini imesema kuwa imefanikiwa kulifanyia majaribio kombora lake la masafa marefu ambalo linaweza kufika eneo lolote la Marekani.
Runinga ya kitaifa nchini humo imesema kuwa Pyongyang sasa imefanikiwa kuafikia azimio lake la kuwa taifa lenye nguvu za kinyuklia.
Kombora hilo kwa jina Hwasong-15 ambalo imesema ndio kombora lenye uwezo mkubwa lilirushwa katika giza mapema siku ya Jumatano.
Lilianguka katika maji ya Japan lakini liliweza kuruka juu zaidi ya kombora jingine lolote la taifa hilo .
Rais wa Marekani Donald Trump ameonya vitisho kutoka kwa mataifa Korea kaskazini na Iran katika hotuba yake katika umoja wa mataifa.
Katika hotuba yake ya kwanza katika mkutano wa umja huo mjini New York, ameonya kuwa Marekani itaangamiza Korea kaskazini iwapo italazimika kujitetea ama kuwalinda washirika wake.
Alimkejeli kiongozi wa Korea kaskazinmi Kim Jong un akisema: Yuko katika harakati za ''kujitoa muhanga''.
Korea kaskazini imefanya makombora yake kinyuklia majaribio na kukiuka maamuzi ya Umoja wa mataifa.
Iran, bwana Trump alisema ni nchi ya kifisadi na inayoongozwa kidikteta kwa lengo la kutaka kuyumbisha eneo la mashariki ya kati.
Jeshi la Marekani limerusha ndege yake ya kuangusha mabomu aina ya B-1B katika anga ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza kushambulia nchini Marekani.
Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya mabomu ya nyuklia.
Taifa la Korea Kaskazini limefanyia majaribio kombora lake la masafa marefu lililoruka juu zaidi na kombora hilo tayari limeonekana kuhatarisha usalama duniani kulingana na waziri wa maswala ya ulinzi nchini Marekani James Mattis.
Jaribio hilo la kombora mapema siku ya Jumatano lilianguka katika maji ya Japan.
Liliruka kwa urefu wa kilomita 4,500 na kusafiri umbali wa kilomita 960 kulingana na jeshi la Korea Kusini.
Ni jaribio la hivi karibuni ambalo limezua hali ya wasiwasi.
Mara ya mwisho kwa taifa hilo kulifanyia jaribio kombora lake ni mwezi Septemba.
Wakati huo, kombora lake la mwisho lilikuwa la sita la nguvu za kinyuklia mwezi huo.
Rais wa Korea Kusini Moon Jae-In ameitaka Marekani kuacha kwa muda mazoezi yake ya kijeshi nchini humo mpaka kumalizika kwa michuano ya Olimpiki itakayofanyika mapema mwakani.
Anasema hii itasaidia pia kuifanya Korea Kaskazini kutotilia shaka uwepo wa wanamichezo wake kwenye michuano hiyo.
Korea Kusini itakua mwenyeji wa michezo hiyo itakayofanyika katika mji wa Pyeongchang mwezi Februari ikiwa ni kilomita 80 kutoka mpaka wake na Korea Kaskazini.
Mapema Canada na Marekani ziliapa kuendeleza mazoezi hayo ili kuisukuma Korea Kaskazini kuachana na mpango wake wa nyuklia.
Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov amedai Marekani ndiyo imekuwa ikiichokoza Korea Kaskazini na kuichochea kuongeza kasi mpango wake wa silaha za nyuklia.
Amepuuzilia mbali wito kutoka kwa balozi wa Marekani katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wa kuvunja uhusiano na Korea Kaskazini.
Hii ni baada ya Pyongyang kufanyia majaribio kombora jingine.
Urusi imekuwa ikisema kwamba vikwazo na hatua nyingine za kuiadhibu Korea Kaskazini haziwezi kufanikiwa. Badala yake imekuwa ikihimiza kuwepo mashauriano.
Marekani imetahadharisha kwamba serikali ya Korea Kaskazini "itaangamizwa kabisa" iwapo vita vitazuka.
Rais Trump ametangaza kwamba Marekani inaiorodhesha Korea Kaskazini kuwa taifa linalofadhili ugaidi miaka tisa baada ya kuondolewa katika orodha hiyo.
Katika mkutano wa baraza la mawaziri rais Trump amesema kuwa hatua hiyo itasababisha kuwekwa kwa vikwazo vikali dhidi ya taifa hilo vinavyotarajiwa kutangazwa siku ya Jumanne.
Lakini waziri wa maswala ya kigeni Rex Tillerson baadaye alikiri kwamba madhara yake hayatakuwa makubwa.
Bwana Trump amelaumu mpango wa kinyuklia wa taifa hilo na ufadhili wa kile amekitaja kuwa vitendo vya ugaidi wa kimataifa.
Akitoa uamuzi huo katika ikulu ya Whitehouse , Trump amesema kuwa hatua hiyo ingetekelezwa kitambo.
Mnamo mwezi Septemba , Marekani ilipendekeza idadi kadhaa ya vikwazo vya Umoja wa kimataifa dhidi ya Korea Kaskazini, ikiwemo marufuku ya mafuta mbali na kupigwa tanji kwa mali ya rais wa taifa hilo Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imemuelezea Rais Trump kuwa mchafuzi wa amani na utulivu wa dunia, ambaye anatamani vita vya nuklia vitokee.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Korea Kaskazini, imekariri nia ya taifa hilo kubaki na silaha zake za nuklia, ikisema silaha hizo zinalinda heshima na uhuru wa nchi.
Matamshi hayo yanasadifiana na mazoezi makubwa ya manuwari za majeshi ya wanamaji, baina ya Marekani na Korea Kusini.
Hii ni mara ya kwanza katika mwongo mzima, ambapo manuwari tatu za Marekani zinazobeba ndege, kuhusika katika mazoezi hayo.
Akiendelea na ziara yake katika bara la Asia, Rais Trump mara kadha, ameionya Korea Kaskazini, kwamba mradi wake wa silaha za nuklia, ni tishio ambalo halitovumiliwa.
Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungua makombora ya Korea Kaskazini, kwa kutumia mitambo ya kijeshi iliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litatungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.
Maafisa kutoka makao makuu ya ulinzi nchini Marekani, wanaamini kuwa uvamizi wa kutumia vikosi vya Marekani vya nchi kavu, itakua njia pekee ya kupata na kudhibiti maeneo ya nyuklia ya Korea Kaskazini.
Ripoti hiyo ilikuja kwenye barua iliyotolea na makao makuu ya ulinzi nchini Marekani, kujibu ombi la bunge la kutaka kufahamu kuhusu maafa yanayoweza kutokea ikiwa mzozo utalipuka na Korea Kaskazini.
Mjumbe wa Korea Kaskazini amesema kuwa silaha za kinyuklia za taifa hilo haziwezi kujadiliwa.
Choe Son Hui amesema kuwa Marekani inafaa kujiandaa kuishi na Korea Kaskazini yenye silaha za kinyuklia.
Amesema kuwa ndio njia pekee ya kuwa na amani ya kudumu kati rasi ya Korea.
Mkurugenzi wa shirika la kijasusi nchini Marekani Mike Pompeo awali alikuwa ameonya kwamba Korea Kaskazini inaweza kuishambulia Marekani na kombora la kinyuklia katika kipindi cha miezi michache ijayo.
Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilimwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Mkurugenzi wa shirika la ujasusi la Marekani CIA Mike Pompeo ametahadharisha kwamba Korea Kaskazini inakaribia sana kuwa na uwezo wa kuishambulia Marekani kwa kombora la nyuklia.
Amesisitiza kwamba taifa hilo bado linapendeleza zaidi kutumia diplomasia na vikwazo lakini amesema kwamba bado wanatafakari uwezekano wa kutumia nguvu za kijeshi.
Korea Kaskazini imekuwa ikidai kwamba tayari ina uwezo wa kuishambulia Marekani.
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.

Post a Comment

 
Top