0
Tetesi:Kocha wa zamani wa Simba mzambia Patrick Phiri anatajwa kuwa miongoni mwa makocha watakaochukua kibarua cha kuifundisha Simba baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Joseph Omog kuoneshwa mlango wa kutokea kufuatia kutupwa nje kwa timu yake kwenye michuano ya kombe la shirikisho Tanzania (Azam Sports Federation Cup).
Habari ambazo shaffihdauda.co.tz imezipata ni kwamba, kwa sasa kuna mchakato unaendelea ndani ya Simba kutafuta kocha ambaye atachukuwa nafasi ya Omog lakini jina la Phiri likipewa kipaumbele katika mchakato huo.
“Ni kweli kwa sasa Simba kwa sasa ipo katika harakati za kuhakikisha kocha mpya anapatikana haraka kuchukua nafasi ya Omog aliyefukuzwa, Patrick Phiri anapewa nafasi kubwa katika mchakato huo kutokana na uzoefu wake kwenye ligi ya Tanzania pamoja na uzoefu ndani ya klabu kwa hiyo anaweza akapewa nafasi” kimeeleza chanzo kutoka ndani ya uongozi wa Simba.
Phiri anakumbukwa kwa kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara bila kufungwa rekodi ambaye ilifikiwa na Joseph Omog wakati akiifundisha Azam iliposhinda ubingwa mwanga 2013.
Phiri aliwahi kushinda ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili 2004/05 na 2009/10
Amewahi kuwa kocha bora wa mwaka Tanzania 2009/10

Post a Comment

 
Top