0
Rais wa Zimbabwe Robert MugabeHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Raia mmoja wa Marekani Bi Martha O'Donovan' mwenye umri wa miaka 25 amefikishwa mahakamani huko mjini Harare ambako anakabiliwa na kosa kuu la madai ya kujaribu kuipendua serkali.
Adhabu ya kosa hilo kwa anaepatikana na hatia ni kifungo cha miaka 20 jela.
Police wanamtuhumu kwamba ndie anayendesha akaunti ya Twitter iitwayo @matigary ambapo muliwekwa maandishi ya kuhujumu na kumkosea heshima rais Robert Mugabe.
Baadhi ya maandishi yaliyo kwenye akaunti hiyo yanasema na nanukuu ''Nchi yaongozwa na mzee mgonjwa mwenye ubinafsi mkubwa''.
Bi O'Donovan -ambae huendesha mtandao wa video za mizaha ya kisiasa amekana madai hayo akisema hayana msingi wowote.
Katika kipindi cha miaka michache iliyopita mamia ya watu wamekamatwa nchini humo baada ya kutoa matamshi ya kumsema vibaya rais Mugabe na kushtakiwa chini ya sheria iliyopitishwa majuzi inayochukulia swala la kumkosoa rais kuwa kitendo cha kihalifu.
Ni hivi majuzi tu ambapo rais Mugabe alimteua waziri ambaye kazi yake inahusika tu na usalama na udhibiti wa kilicho mitandaoni kinachoihusu Zimbabwe.

Post a Comment

 
Top