Hatimaye Rais Uhuru Kenyatta ameapishwa rasmi kwa muhula wa pili wa miaka mitano katika sherehe zilizofana kwenye Uwanja wa Kasarani mwezi mmoja baada ya kuibuka mshindi wa uchaguzi uliosusiwa na mpinzani mkuu Raila Odinga.
Kulikuwa na nderemo na shangwe katika uwanja huo kutoka kwa maelfu ya wananchi wengi wao wafuasi wa muungano wa chama tawala cha Jubilee waliojaa kwenye Uwanja wa Michezo wa Kimataifa wa Moi, Kasarani.
Uwanja huo unaingiza watu 60,000 lakini habari zinasema walioingia walikuwa 100,000. Wageni waalikwa na watu mashuhuri wapatao 40 walihudhuria sherehe hizo wakiwemo zaidi ya viongozi wakuu wa nchi 10.
Kenyatta, 55, alishinda uchaguzi mkuu wa marudio wa Oktoba 26 kwa asilimia 98. Uchaguzi huo ulifanyika baada ya matokeo ya ushindi wa Agosti 8 kufutwa na Mahakama ya Juu kwa maombi ya Odinga aliyewasilisha ushahidi wa dosari na ukiukwaji wa katiba.
Post a Comment