0
Wahitimu wa kidato cha nne 2017 wa shule ya sekondari Nicodemus Banduka wakiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kwenye mahafari ya 9 yaliyofanyika oktoba 7 shuleni hapo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye meza kuu wakifatilia burudani mbalimbali zilizoweza kuburudishwa kwenye mahafari 
Wanafunzi Shija Kinoga (katikati) akisoma lisala kwa niaba ya wanafunzi wa kidato cha nne mwaka 2017 katika shule ya sekondari Nicodemus Banduka.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Joseph Sika akizungumza kwenye mahafari ya 9 ya kidato cha nne mwaka 2017.
Mgeni rasmi ambaye ni Afisa elimu taluma sekondari wilaya, Malima Msilanga akzingumza na wazazi pamoja na walezi kwenye mahafari ya tisa ya kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari ya Nicodemus Banduka 
 Wahitimu wa kidato cha nne 2017 wakifatilia hutuba ya mgeni rasmi kwa umakini

Wazazi pamoja na walezi waliweza kujitokeza kwa wingi kuja kusikiliza ujumbe kwenye mahafari ya 9 ya kidato cha nne mwaka 2017
 Wahitimu wakiwa wameshika vyeti vya kuhitimu kidato cha nne

Wazazi na walezi wametakiwa kuwahimiza wanafunzi kuhudhulia masomo ipasavyo na kufuatilia kwa ukaribu maendeleo ya wanafunzi kipindi wawapo shuleni ili kuweza kukomesha utoro na kuweza kuongeza ufaulu.

Wito huo umetolewa jana oktoba 7 na mgeni rasmi ambaye ni Afisa elimu taluma sekondari wilaya, Malima Msilanga akzingumza na wazazi pamoja na walezi kwenye mahafari ya tisa ya kidato cha nne 2017 katika shule ya sekondari ya Nicodemus Banduka iliypoto kata ya Mbaya wilaya ya Liwale mkoani Lindi.

Msilanga amesema licha ya sekondari hiyo kufanya vizuri kitaaluma mwaka 2016 lakini shule hiyo inachangamoto ya utoro hali inayopelekea watoro hao kufanya vibaya kwenye mtihani hao wa kuhitimu kidato cha nne kwakuwa hawaudhulii vipindi ipasavyo.

Awali mwanafunzi Shija Kinoga akisoma lisala kwa niaba ya wahitimu wa kidato cha nne kwa mgeni rasmi katika lisala hiyo alibainisha kuwa idadi ya wanaohitimu imekuwa ndogo ikiwa wanafunzi 26,wavulana 14 na wasichana 12 ukilinganisha na idadi ya wanafunzi walioanza kidato cha kwanza walikuwa 98 .

Katika lisala hiyo ilieleza kuwa walipokuwa shuleni hapo wamejifunza mambo mbalimbali kama shughuli ya kilimo,kuepuka vitendo vya ushawishi vya mitaani,kujituma,kukataza mambo mabaya na kuhimiza matendo mema.

Licha ya kueleza mafanyikio lakini kuna baadhi ya changamoto wa shuleni hapo ikiwa uhaba wa walimu wa masomo ya sayansi ikiwa hisabati na chemia,uhaba wa nyumba za walimu,maji,choo,uchakavu wa miundombinu pamoja na umeme kutoka na changamoto hizo zinachangia wanafunzi kukwama kutimiza ndoto zao.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa sekondari, Joseph Sika alisema wao kama walimu wametimiza majukumu yao ya kuwafundisha na moja ya kipimo cha wanafunzi hao waliweza kufanya mtihani wa kujipima Mock wilaya baada ya matokeo shule hiyo ilishika nafasi ya 3 kiwilaya kati ya shule 16.

Mratibu elimu kata ya Mbaya, Dionis Mbilinyi amewahadi wahitimu hao wa kidato cha nne 2017 mwanafunzi yeyote atakae faulu na kuendelea na kidato cha tano ataweza kumchangia shilingi elfu hamsani (50,000/=).

Post a Comment

 
Top