Ndugu Hasani Mpako (kushoto) akiwa nahodha wa Leopard fc,Ramadhani Ngunduli pamoja na mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe. Sarah Chiwamba wakimkabidhi nahodha wa timu ya Leopard fc kombe baada ya kuichapa timu ya Hawili fc kwa mikwaju ya penaiti 6-5.
Nahodha wa Hawili fc, Uwesu Mbala akipokea zawadi kwa niaba ya timu yake mara baada ya kushindwa kutetea kombe mwaka 2017 na kukubali kufungwa kwa mikwaju ya penaiti ya 6-5 kati ya penaiti 8 zilizopigwa kila upande.
Mchezaji wa muda mrefu toka mwaka 2001-2017 ambaye hajawahi kupewa kadi nyekundi na mwenye nidhamu ni Shabani Mbwani kutoka Mitumba fc akitunukiwa cheti kutoka TFF pamoja na fedha shilingi 20,000
Mratibu wa mashindano hayo, Selemani Nangomwa akisoma risala
Mchezaji wa muda mrefu toka mwaka 2001-2017 ambaye hajawahi kupewa kadi nyekundi na mwenye nidhamu ni Shabani Mbwani kutoka Mitumba fc akitunukiwa cheti kutoka TFF pamoja na fedha shilingi 20,000
Mratibu wa mashindano hayo, Selemani Nangomwa akisoma risala
TIMU ya Leopard FC imetawazwa kuwa mabingwa wapya wa Ligi ya Alizeti cup 2017 leo oktoba 27 baada ya kuicha Hawili fc kwa mikwaju ya penaiti 6-5 kati ya penaiti 8 zilizopigwa kwenye Uwanja wa Halmashauri ya wilaya Liwale mkoani Lindi.
Lakini Hawili ilionekana kupania mchezo huo lakini timu ya Leopard fc ilianza kupata bao la kuongoza kupitia kwa Buruhani Ngahata dakika ya 29 na Hawili fc waliweza kusawazisha goli hilo na Huseni Mchite namo dakika ya 35 na matokeo hayo yalipelekea mpaka dakika 90 za mchezo.
Liwale Blog ilizungumza na Nahodha wa Leopard fc,Ramadhani Ngunduli alisema mchezo ulikuwa mgumu toka dakika za mwanzo Lakini alikiri ugumu wa mashindano hayo mwaka huu. Kwa upande wa Nahodha wa Hawili, Uwesu Mbala alisema mchezo huo ulikuwa mgumu kwa pande zote katika dakika 90 na hatua ya mikwaju ya penaiti bahati iliangukia kwa Leopard fc.
Nao wadhamini wa ligi hiyo ambao ni Chama cha Msingi Umoja (Umoja Amcos) chini ya Mwenyekiti, Hasani Mpako alisema ligi hiyo ilikuwa na lengo kuu ni kuwahamasisha wakulima, walime zao jipya la Alizeti katika wilaya ya Liwale na aliongeza kusema ligi litakuwa endelevu kila mwaka mpaka pale uzalishaji wa zao la alizeti litakapopanda angalau kufikia tani 500.
Mratibu wa mashindano hayo, Selemani Nangomwa akisoma risala kwa mgeni rasmi alibainisha kuwa Umoja Amcos kimeweza kufunga mtambo wa kukamulia mafuta na kitanunua alizeti zote itakayolimwa katika wilaya hii.
Kwa upande wa mgeni rasmi ambaye ni mkuu wa wilaya ya Liwale,mhe.Sarah Chiwamba alitumia nafasi hiyo kuwahasa vijana kujiunga na vilabu vya mpira ili kuweza kujiepusha na vitendo vibaya kwani aliongeza kusema mchezo ni afya na michezo ni moja ya ajira pia aliwaomba wananchi kuhamasika kulima zao la aliziti ili kuweza kuongeza kipato.
Zawadi zilikuwa za mtu mmoja mmoja kama mchezaji bora Lawrance Fusi kutoka Leopard fc,golikipa bora Shabani Matenula kutoka Leopard fc ,mfungaji bora Ikramu Kanunga kutoka New vision fc na mchezaji wa muda mrefu na mwenye nidhamu ni Shabani Mbwani kutoka Mitumba fc alipewa cheti kutoka Tff na waliweza kuzawadiwa shilingi 20000 kila mmoja.
Mshindi wa tatu alipewa shilingi 300,000 na jezi seti moja ,mshindi wa pili alipewa shilingi 500,000 na jezi seti moja na bingwa alijinyakulia shilingi 1,000,000,jezi seti moja na kombe lenye thamani ya shilingi 350,000
Ligi la alizeti cup 2017 lilishirikisha zaidi ya timu 27 kutoka vituo mbalimbali vilivyopambwa na waratibu wa mashindano haya na hatua ya nane bora ziliweza kucheza katika uwanja wa wilaya ya Liwale mkoani Lindi.
Post a Comment