Jonas Kamaleki- MAELEZO
Serikali imewataka wataalam wa mipangomiji kuandaa mwongozo wa upimaji wa mitaa na vijiji maeneo ya vijijini ili kuboresha makazi.
Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Wiliam Lukuvi wakati akifungua Mkutano wa Nne wa Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji (TPRB).
Waziri Lukuvi amewataka pia wataalam hao watengeneze mwongozo wa kuharakisha urasmishaji wa makazi holela. “Nataka mtengeneze mwongozo wa uendelezaji fukwe na kuangalia namna ya kurekebisha sheria zinazokinzana,” alisema Lukuvi.
Aidha, Lukuvi amewataka wapangamiji kuandaa mpango mwepesi wa kuondoa urasimu wa utoaji wa vibali vya ujenzi ili kuwaondolea adha wananchi ambao pengine wanakopa ili wajenge na kufanya biashara. Amependekeza vibali vya ujenzi vitolewe ndani ya mwezi mmoja au hata wiki moja itoshe kutoa vibali hivyo ili kuondokana na urasimu katika ujenzi.
Wale waliojenga kwenye maeneo yaliyopimwa lakini hawana vibali vya ujenzi, Lukuvi amesema wasisumbuliwe kwani watoa vibali ndio waliowachelewesha. Ameongeza kuwa kwa waliojenga kwenye maeneo yasiyopimwa, maeneo yao yarasimishwe.
Kuhusu ajenzi wa uchumi wa viwanda, Waziri Lukuvi amesema upangaji miji uzingatie kutenga maeneo kwa ajli ya ujenzi wa viwanda katika miji na Halmashauri zote nchini. Lukuvi amesema wapangamiji wazingatie pia miundombinu ya umeme, maji, maeneo ya huduma kama makaburi, maaeneo ya wazi, shule na maeneo ya ibada.
Waziri amewataka watumishi wa Serikali wa mipangomiji wasiowaadilifu wachukuliwe hatua kali za kisheria na TPRB. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wataalam wa Mipangomiji, Prof. Wilbroad Komba amesema kuwa Bodi inajitahidi kufanya kazi zake kwa weledi licha ya changamoto ya kuwa na wataalam wachache.
Tanzania inao wataalam wa mipangomiji 306 waliosajiliwa ambao ni asilimia 25 tu kati ya wale wanaohitajika kwa shughuli za kupanga miji.
Mkutano huo wa Nne wa Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji una kaulimbiu isemayo: “Mipangomiji na Uchumi wa Viwanda.”

Post a Comment